Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mwenyekiti
wa Baraza la Usalama Barabarani, Pereira Ame Silima akizungumza na Wadau wa
Usalama Barabarani pamoja na Wajumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani
kutoka mikoa yote nchini katika mkutano wa baraza hilo ambao unajadili masuala
mbalimbali ya jinsi ya kupunguza ajali za barabarani nchini. Kulia ni Katibu wa
Baraza la Usalama Barabarani ambaye pia ni Kamanda wa Kikosi cha Polisi Usalama
Barabarani nchini, Naibu Kamishna wa Polisi, Mohamed Mpinga. Katikati ni Kamishna
Msaidizi wa Jeshi la Polisi nchini Malawi ambaye pia ni Kiongozi wa Kikosi cha
Usalama Barabarani nchini humo, Maepheson Matowe. Mkutano huo ambao unaenda sambamba na
Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani unafanyika katika Hoteli ya
Regal Naivera jijini Tanga leo. Picha
zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Sehemu ya Wadau na Wajumbe wa Baraza la Usalama
Barabarani kutoka mikoa yote chini wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa
Baraza hilo, Pereira Ame Silima (hayupo pichani) katika mkutano wa baraza hilo
ambao unajadili masuala mbalimbali ya jinsi ya kupunguza ajali za barabarani
nchini. Mkutano huo unaenda sambamba na Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama
Barabarani unafanyika katika Hoteli ya Regal Naivera jijini Tanga leo . Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi.
Mtoa mada wa Mkutano Mkuu wa Wadau wa Usalama
Barabarani ambaye ni Mkemia Mkuu wa Serikali, Prof. Samweli Manyele akizungumza
na Wadau wa Usalama Barabarani pamoja na Wajumbe wa Baraza la Taifa la Usalama
Barabarani kutoka mikoa yote nchini katika mkutano wa baraza hilo ambao
unajadili masuala mbalimbali ya jinsi ya kupunguza ajali za barabarani nchini.
Prof. Manyele alitoa elimu ya jinsi ya kusafirisha salama kemikali. Mkutano huo
ambao unaenda sambamba na Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani
unafanyika katika Hoteli ya Regal Naivera jijini Tanga leo. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mwenyekiti
wa Baraza la Usalama Barabarani, Pereira Ame Silima (katikati meza kuu) akijadili
jambo na Kamanda wa Kikosi cha Polisi Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna
wa Polisi, Mohamed Mpinga, wakati wa Mkutano Mkuu wa Wadau wa Usalama
Barabarani pamoja na Wajumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani kutoka
mikoa yote nchini katika mkutano wa baraza hilo ambao unajadili masuala
mbalimbali ya jinsi ya kupunguza ajali za barabarani nchini. Wengine katika
picha ni wajumbe wa mkutano huo. Mkutano huo ambao unaenda sambamba na
Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani unafanyika katika Hoteli ya
Regal Naivera jijini Tanga leo. Picha
zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
KITENGO CHA
MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO
YA NDANI YA NCHI.
No comments:
Post a Comment