Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imewasili salama leo
asubuhi jijini Mwanza, tayari kwa maandalizi ya mchezo wa kirafiki wa Kimataifa
siku ya jumapili Machi 29, 2015 dhidi ya timu ya Taifa ya Malawi (The Flames),
mechi itakayochezwa kwenye dimba la Uwanja wa CCM Kirumba.
Kikosi cha Stars kimeondoka kikiwa na wachezaji 18 ambao
wameripoti kambini jana, huku kiugo mshambuliaji Mwinyi Kazimoto anayecheza
soka la kulipwa nchini Qatar akitarajiwa kuungana na wenzake leo mchana jijini
Mwanza.
Wachezaji waliopo kambini jijini Mwanza ni, magolikipa Aishi
Manula na Mwadini Ali (Azam FC), walinzi ni Erasto Nyoni, Shomary Kapombe,
Aggrey Morris (Azam FC) , Salim Mbonde (Mtibwa Sugar), Haji Mwinyi (KMKM),
Hassan Isihaka na Abdi Banda (Simba SC)
Wengine ni Amri Kiemba, Frank Domayo, Salum Abubakar (Azam
FC), Said Ndemla (Simba SC), Haroun Chanongo (Stand United), John Bocco (Azam
FC), Juma Luizio (Zesco United), Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu (TP
Mazembe).
Mchezaji Mcha Khamis wa Azam FC amejiondoa kikosini kutokana
na kuwa majeruhi, huku wachezaji wa Young Africans wakitarajiwa kujiunga na
kikosi hicho cha timu ya Taifa mara tu baada ya mchezo wao wa Ligi Kuu ya
Vodacom dhidi ya JKT Ruvu siku ya jumatano.
No comments:
Post a Comment