Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Saturday, 28 March 2015

CCM WAASWA KACHANA NA MAKUNDI


Na Hastin Liumba,TaboraMJUMBE wa mkutano mkuu wa CCM taifa Emmanuel Mwakasaka amewaasa wanachama wenzake kuachana na makundi ndani ya chama hicho kwani yanajenga chuki na kuweza kusambaratisha chama.


Mwakasaka alitoa kauli hiyo wakati akiongea na wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM wilaya ya Tabora mjini mara baada ya kuchaguliwa katika nafasi hiyo.

Mwakasaka alisema siku zote huwa hapendi makundi ndani vyama na kwamba anaamini huwa hayana tija zaidi ya kuleta mifarakano,chuki na hata kutishia uhai wa chama chenyewe.

Alisema makundi hayapo tu CCM bali vyama vyote hivyo ni wajibu wanachama na viongozi kushikamana ili kujenga umoja na utaifa zaidi.

Alisema makundi ndani ya vyama mara nyingi yanasababisha mipasuko na kuhatarisha mustakabali wa taifa kwani viashiria vya vita viko wazi na ufike wakati tutambue hilo.

Kuhusu nafasi aliyochaguliwa ya mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM taifa Mwakasaka alisema ana deni na wanachama wenzake na wananchi kwa ujumla.

“Unapochaguliwa kwenye nafasi yoyote ile wale waliokuchagua wana imani nawe….hivyo mimi ninahidi nitafanya kazi itakayotokana na kuchaguliwa kwangu,” alisema.

Alisema uchaguzi siku zote anayechaguliwa ni mtu anayefaa hivyo kama ameonekana anafaa basi atashirikiana na watu wote bila kujali itikadi za vyama.

Kuhusu uchaguzi huo msimamizi wa uchaguzi katibu wa CCM wilaya ya Tabora mjini Bakar Lwasa akitangaza matokeo hayo alisema kura zilizopigwa zilikuwa 146 na Emmanuel Mwakasaka alipata kura (130).

Alisema wagombe wengine aliyefuatia Joyce Ndonde kura (5), Rhoda Sangwa (4), Kapele Baridi (4), Said Humbi (2), Tatu Mkilya (1), Ali Mwantende (0), Rose Kilimba (0), Pili Kassim (0) na Jane Kabeho (0).

No comments:

Post a Comment