Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Monday 30 March 2015

SAMATTA AIOKOA TAIFA STARS MWANZA

  Mshambuliaji wa Tanzania 'Taifa Stars ' Mbwana Samata (kushoto) akiwania mpira na beki wa Malawi ,John Lanyesi wakati wa mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliozikutanisha timu timu hizo kwenye uwanja wa CCM Kirumba , Mwanza jana.Timu hizo zilitoka sare 1-1.Picha na Michael Jamson.  

Mshambuliaji kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samata ameibuka shujaa baada ya kuifungia bao Taifa Stars ikilazimishwa sare 1-1 na Malawi katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza jana.

Malawi ilianza mchezo kwa kasi na kufanikiwa kupata bao la kuongoza dakika ya tatu lililofungwa na Mihum Mphone aliyemalizia mpira ulioshindwa kuokolewa na mabeki wa Taifa Stars baada ya kona ya iliyopigwa na John Banda. Bao hilo liliwaondoa Stars mchezoni kwani katika dakika 10 za mwanzo ilicheza bila ya malengo na kuwapa nafasi kubwa Malawi kutalawa mchezo huo.

Dakika ya 14, Samata nusura aisawazishie Stars baada ya kupiga shuti akiwa nje ya eneo la 18, lililopanguliwa na kipa Donald Harawa na kuwa kona ambayo haikuzaa matunda.

Thomas Ulimwengu alikosa bao dakika 22, baada ya shuti lake kuokolewa na kipa Harawa katika uwanja huo uliojaa tope na maji kutokana na mvua kubwa iliyoonyesha jijini Mwanza.

Malawi ilikwenda mapumziko ikiwa mbele 1-0, pamoja na kutawala sehemu kubwa mchezo hasa katika eneo la kiungo.

Taifa Stars ilirudi kipindi cha pili kwa nguvu baada ya kocha Mart Nooij kuwapumzisha Haruna Chanongo, Amri Kiemba na Ulimwengu na kuwaingiza Mrisho Ngassa, Abubakari Salum ‘Sure Boy’, na John Bocco.

Mabadiliko hayo yaliifanya Stars kutawala katikati ya uwanja na kuanza kufanya mashambulizi mengi langoni kwa Malawi walioaamua kucheza kwa kujilinda.

Dakika ya 75 krosi ya Ngassa ilimkuta Samata aliyepiga shuti lililokwenda moja kwa moja wavuni na kuisawazishia Stars katika dakika 75, bao hilo liliamsha shangwe za mashabiki wa Tanzania waliojitokeza uwanjani hapo.

Bocco naye nusura apate bao katika dakika 80, baada ya shuti lake kupaa juu kidogo ya lango la Malawi.

Kocha wa Stars, Nooij alisema Malawi ni timu nzuri ina wachezaji bora, lakini wachezaji wake walifanya kosa kuruhusu kufungwa bao la mapema.

Naye kocha wa Malawi, Chimuzi Yangi alisema mchezo ulikuwa mgumu na wachezaji wake walicheza vizuri, ila kosa moja walililolifanya limewaghalimu.


Kufuzu CHAN 2016
Taifa Stars itaanza kampeni yake ya kusaka kufuzu kwa fainali za Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) Rwanda 2016 hapo Juni 19-21.
Kwa mujibu wa taarifa ya Shirikisho la Soka Afrikca (CAF) ratiba ya mashindano hayo itapangwa Aprili 5, jijini Cairo, Misri.
Mashindano ya CHAN yatashirikisha timu 42, ambazo zitapangwa kushindana kutokana na kanda sita za nchi wanachama wa CAF.
Mechi za mtoano zitaanza kuanzia Juni 19-21 zitafanyika hadi Agosti 28-30 ambako zitapatikana timu 15, zitakazoungana na wenyeji Rwanda tayari kwa fainali zitakazoanza Januari 16 hadi Februari 7, 2016.
Washindi wa fainali tatu zilizopita za CHAN, ni DR Congo (2009), Tunisia (2011) na Libya (2014).
Taifa Stars: Mwadini Ally, Shomari Kapombe, Oscar Joshua, Agrey Morris, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Erasto Nyoni, Mwinyi Kazimoto, Amri Kiemba, Thomas Ulimwengu/John Bocco (dk. 81), Mbwana Samata na Haroun Chanongo/Mrisho Ngassa (dk. 59).
Malawi: Mcdonald Harawa, Joseph Kamwendo, John Lanjesi, Harry Nyirenda, Limbikani Mzava, Chimango Kaira, Francis Mulimbika, John Banda, Mucium Mhone, Peter Wadabwa na Essau Kanyenda.

CREDIT: MWANANCHI

No comments:

Post a Comment