Nigeria ndio mabingwa wa mwaka huu wa taji la Afrika la Vijana wasiozidi umri wa miaka 20.
Nigeria ilitawazwa mabingwa baada ya kuinyuka Senegal bao moja kwa nunge katika fainali za mashindano hayo yaliyoandaliwa huko Dakar.
Kiungo cha kati wa ''The Flying Eagles'' Bernard Bulbwa ndiye aliyepachika bao hilo katika kipindi cha kwanza.
Kufuatia ushindi huo Nigeria sasa wamewazidi wapinzani wao Misri kwa zaidi ya mataji matatu.
Timu hiyo ya Nigeria inaungana na Senegal, Ghana na Mali kuiwakilisha Afrika katika kombe la dunia la vijana wasiozidi umri wa miaka 20 .
The Flying Eagles wamejumuishwa kwenye kundi E ambapo wanatarajiwa kujiunga na Brazil, Korea Kaskazinina Hungary.
Mashindano hayo yataaanza mei tarehe 30na kukamilika juni tarehe 20 huko New Zealand.
Senegal, Ghana na Mali walifahamishwa wapinzani wao mapema leo.
Ghana iko katika kundi Ba kwa pamoja na Argentina, Panama na Austria.
Senegal itakabiliana na Qatar, Colombia na Portugal katika kundi C.
Mali Kwa upande wake itachuana dhidi ya Mexico, Uruguay na Serbia katika kundi D.
CREDIT: BBC
No comments:
Post a Comment