Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday, 26 March 2015

MADAKTARI BINGWA WAWASILI TABORA


Na Hastin Liumba, Tabora

JUMLA ya madaktari bingwa watano (5) kutoka nchi za Switzerland (Uswisi) na Ujerumani wamewasili mkoani Tabora kwa ajili ya kuanza rasmi kampeni ya uchunguzi wa magonjwa ya tezi dume na ngiri kwa wanaume.


Madaktari hao bingwa waliwasili mjini hapa na wametambulishwa kwa Kaimu Mkuu wa Mkoa huo Suleiman Kumchaya kabla ya kupelekwa katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa huo, Kitete ili kuanza kampeni hiyo itakayochukua muda wa wiki mbili.

Akitoa neno la ukaribisho kwa wageni hao Kumchaya alisema serikali imefurahishwa na ujio wao na wanamatarajio makubwa wananchi wote wenye matatizo hayo au watakaobainika katika uchunguzi huo watapatiwa matibabu stahiki ikiwemo kufanyiwa upasuaji.

Alisema ni jambo la kujivunia kwa mkoa huo kupata fursa hiyo ya kipekee kwa wananchi wake kufanyiwa uchunguzi wa matatizo hayo na kisha wahusika kufanyiwa upasuaji, kwani zoezi hili litarudisha afya za wananchi wengi katika hali ya kawaida.

Kaimu Mganga Mkuu wa mkoa wa Tabora Dr Fikiri Martin alisema kampeni hii ni muhimu  hapa nchini na hususani katika mkoa huo kwani viashiria vya awali vimeonyesha dhahiri uwepo wa wanaume wenye matatizo ya tezi dume na ngiri hivyo suala la uchunguzi ni la muhimu.

Alifafanua kampeni hiyo gharama ya upasuaji wa ngiri kwa mgonjwa mmoja itakuwa sh 50,000 ambayo ni sawa na nusu ya gharama ya kawaida ya upasuaji ya sh 100,000 na kuongeza gharama ya uchunguzi wa tatizo la tezi dume itategemea idadi ya vipimo, aina na hatua ya tezi dume iliyofikia.

Aidha alisema madaktari hao watatoa mafunzo maalumu kwa watumishi wa afya katika hospitali hiyo ya mkoa na wale wa manispaa na pia watakabidhi msaada wa vifaa tiba na dawa kwa uongozi wa hospitali
hiyo.

No comments:

Post a Comment