Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday 31 March 2015

WAUMINI KANISA KCC WATOA MSAADA KWA MLEMAVU

Na Hastin Liumba, Tabora
WAUMINI kanisa la Tanzania Assemblies of God tawi la Kitete Christian Center (KCC)  wametoa msaada wa baiskeli (wheel chair) yenye thamani ya Sh 355,000.



Msaada huo ulitolewa kwa Jeremia Sadoki (30) mwenye ulemavu wa miguu yote miwili ikiwa ni baiskeli ya thamani ya Sh 300,000 na fedha taslimu Sh 55,000.

Msaada huo ulitolewa wakati wa ibada baada ya kukamilika kwa zoezi la ukusanyaji michango ya waumini wa kanisa kwa ajili ya kumsaidia kijana huyo mlemavu ambaye ni mkazi wa kijiji cha Ussoke wilaya ya Urambo mkoani Tabora.

Katika harambee yao waumini hao walifanikiwa kukusanya kiasi cha Sh. 532,000 zilizotolewa kama sadaka maalumu kwa ajili ya kumsaidia kijana huyo.

Mara baada ya kukusanya michango hiyo Mwenyekiti wa harambee hiyo Mayaya Nshimba alijitolea kwenda Dar es salaam kununua baiskeli hiyo na vitu vinginevyo ili waweze kumkabidhi mlengwa huyo.

Akikabidhi msaada huo kwa niaba ya waumini wa kanisa hilo Askofu Paul Meivukie wa jimbo la Tabora aliwashukuru waumini hao kwa moyo wao wa upendo na utayari wao wa kutoa fedha, mali na vitu mbalimbali pasipokujali gharama kwa ajili ya kuisaidia jamii yenye uhitaji.

Askofu alimkabidhi kijana huyo baiskeli ya miguu mitatu (wheel-chair) yenye thamani  ya

Baada ya kupokea vifaa hivyo dada wa Jeremia aliwashukuru waumini wote wa kanisa hilo la KCC kwa jinsi walivyojitoa kwa kiwango kikubwa kuchanga fedha zao na kununua vituo hivyo.

‘Ndugu zangu nawashukuruni sana kwa msaada wenu, naomba Mungu awabariki, mmetusaidia sana wala tusingeweza kununua baiskeli hiyo’, aliongeza.

No comments:

Post a Comment