Kamati ya
mashindano ya Chama cha Soka Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA),iliyokaa kikao chake
15/03/2015 kupitoia rufaa mbalimbali kwa vilabu vinavyoshiriki ligi ya mkoa wa
Dar es salaam, imetoa uamuzi wa kuitupilia mbali rufaa ya FFU FC dhidi ya SHABAB
SC, wakilalamikiwa kuwachezesha wachezaji wawili
kinyume na kanuni.
wachezaji
hao wanaolalamikiwa ni RAMADHAN TUGA na YAKUB,walioitumikia klabu ya Shabab
katika mchezo uliopigwa 10/03/2015,mchezo namba 52,na wakati huohuo
wakiitumikia klabu ya Ashanti United ya Ilala katika michuano ya ligi daraja la
kwanza msimu huu 2014/2015.
kamati baada
ya kupitia vielelezo mbalimbali vilivyowasilishwa na Pan Africa,Ripoti ya
mwamuzi,ripoti ya kamisaa na taarifa za usajili wa Shabab,haikuona sababu ya
kubatilisha matokeo hayo ya mchezo husika ,hivyo kamati imeamua matokeo
yatabaki kama yalivyotokea uwanjani kwa timu hizo kufungana bao 1-1.
aidha kamati
inatoa fursa kwa klabu ya Pan Africa kukata rufaa katika ngazi za juu kama
hawakuridhika na uamuzi wa kamati.
WAKATI HUO HUO ,kamati imetoa uamuzi wa kuipa
ushindi wa magoli 3 na pointi 3 klabu ya FFU,baada ya kushinda rufaa yake dhidi
ya Sinza Stars wanaolalamikiwa kuwatumia wachezaji waliotumia majina yasiyokuwa yao,wachezaji
hao ni Waziri Mwenzemba na Noel Ndemla,ambao majina yao kamili ni (Waziri
Mwanzemba ni Tumain Agustino,na Noel Ndemla ni Mussa Hamis Ndiyunze)
wachezaji
hao usajili wao upo katika vilabu vya JKT Ruvu na wakapelekwa Villa Squad kwa
mkopo kuitumikia klabu hiyo katika michuano ya ligi daraja la kwanza msiamu
2014/2015.
KATIKA HATUA NYINGINE,mchezo wa mtoano wa kutafuta timu
itakayoungana na timu mbili zilizofanikiwa kuingia ligi ya mabingwa mkoa
itapigwa 26/03/2015 katika uwanja wa Mizinga Kigamboni,ukizikutanisha timu za
Pan Africa dhidi ya Changanyikeni.
mshindi
katika mchezo huo ataungana na timu za Zakhem na FFC.
KASONGO
AWAFAGILIA TWIGA STARS.
mwenyekiti
wa DRFA Almas Kasongo,amewapongeza wachezaji wa timu ya soka ya wanawake Twiga
Stars kwa mwanzo mzuri wa kuifunga timu ya taifa ya Zambia kwa mabo 4-2,katika
mchezo wa marudiano uliopigwa huko Zambia.
No comments:
Post a Comment