Wachimbaji wadogo
Na Hastin Liumba, Nzega
CHAMA chama cha wachimbaji wadogo wa madini mkoa wa Tabora (TABOREMA) hatimaye kimepata uongozi mpya.
Chama hicho sasa kitaongozwa na mwenyekiti wake Rashidi Shaout baada ya kufariki dunia kwa aliyekuwa mwenyekiti wa awali Joseph Masolwa.
AKizungumza baada ya kutangazwa mshindi Shabout alisema kwa muda mrefu wachimbaji wadogo wa madini wa mkoa wa Tabora walikosa mwenyekiti wa chama hicho hali iliyopelekea kushindwa kutekeleza na kutatua matatizo ya wananchama hao kwa muda.
Alisema kwa sasa wachimbaji wadogo watapata fursa ya kuonana na mwenyekiti ikiwa na kutatua kero mbalimbali ambazo zilishindwa kutatuliwa kwa muda muafaka na kuongeza kuwa wachimbaji hao wanapaswa kutii sheria bila shuruti.
Aliwataka viongozi wengine wa chama hicho kuongeza ushirikiano wa utendaji kazi ikiwa na kuwatembelea wachimbaji wadogo katika migodi yao ilikubaini matatizo ambayo yanaweza kutatuliwa kwa haraka.
Alisema chama hicho kilikuwa kikikabiliwa na changamoto ya nafasi ya mwenyekiti hali iliyopelekea kushindwa kufanya kazi zake kwa ufanisi ambapo kwa sasa kinatarajia kutatua matatizo ya wachimbaji wadogo ikiwa na kuishawishi serikali kutoa leseni za viwanja vya madini.
Mjumbe wa mkutano mkuu mkoa Maulidi Mtumba amekitaka chama hicho kuhakikisha kinatatua matatizo ya wachimbaji kwa muda muafaka na kuutaka uongozi kutoa mafunzo mbalimbali kwa wachimbaji.
No comments:
Post a Comment