Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Wednesday 25 March 2015

HATARI: AWAUA WANAWE NA KUWAEKA NDANI YA JOKOFU



Mwanamke mmoja amekamatwa na polisi kufuatia mauaji ya wanawe wawili waliopatikana wamefungikiwa ndani ya jokofu.

Maafisa wa polisi wanasema kuwa mwanamke huyo mama wa watoto wanne aliwatumbukiza wanawe wawili wenye umri wa miaka 11 na mwengine mwenye umri wa miaka 14 ndani ya jokofu baada ya kuwaua.
Aidha miili ya mvulana 11, na msichana 14, ilipatikana imewekwa kwenye karatasi za plastiki ilizisivunde.
Yamkini miili hiyo ilipatikana na maafisa wa idara ya mahakama waliokwenda nyumbani kwa mama huyo kwa nia ya kumfurusha baada ya kushindwa kugharamia kodi ya nyumba .
Walishtuka kupata miili ya watoto hao na mara moja wakawaarifu maafisa wa polisi katika jimbo hilo.
Wanawe wawili waliosalia walikuwa kwa jirani na walichukuliwa na kupewa usalama.
Uchunguzi na upasuaji wa maiti unatarajiwa kufanyika ilikubaina kiini haswa cha vifo vyao.
Afisa mkuu wa polisi katika jimbo hilo James Craig ametaja kitendo cha mwanamke huyo kuwa cha kuogofya mno.
Jirani ya mwanamke huyo Tori Childs, aliliambia shirika la habari la AP kuwa watoto hao wawili waliopatikana walikuwa wametoweka kwa takriban mwaka mzima .
Majirani wengine walisema kuwa mwanamke huyo alikuwa taabani haswa baada ya kushindwa kulipa kodi ya nyumba, na kuwa mama huyo mwenye umri wa miaka 36 alikuwa kanakwamba anakabiliwa na upungufu fulani maishani mwake.
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment