Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Saturday 28 March 2015

AWEKWA MOYO WA MAREHEMU


Madaktari wa upasuaji huko Cambridgeshire wamefanya upandikizaji wa kwanza wa moyo barani Ulaya kwa kutumia moyo mwingine uliosimama kufanya kazi.

Mioyo hiyo hupatikana kutoka kwa watu waliokufa lakini ambao mioyo yao bado inafanya kazi.
Katika upasuaji huo,moyo huo ulitoka kwa mtu ambaye mapafu yake na moyo wake ulikuwa haufanyi kazi.
Hospitali ya Papworth inasema kuwa mbinu hiyo huenda ikaongeza idadi ya mioyo inayopatikana kwa asilimia 25.
Mgonjwa aliyewekwa moyo mpya kwa jina Huseyin Ulucan, mwenye umri wa miaka 60, kutoka London,alikabiliwa na shinikizo la moyo mwaka 2008.
Alisema: kabla ya upasuaji,sikuweza kutembea na nilichoka sana, kwa hakika siku na maisha mazuri.
Upandikizaji wa moyo
Lakini anasema kuwa amefurahishwa na kuimarika kwa afya yake tangu upandikizaji huo.
Kwa sasa najisikia mwenye nguvu kila siku,na nimetembea hadi haospitalini asubuhi hii bila tatizo.
Kumekuwa na visa 171 vya upandikizaji wa myoyo katika kipindi cha miaka 12 iliopita nchini Uingereza.
Lakini mahitaji yanashinda myoyo iliopo ,hivyobasi wagonjwa wengine hungoja kwa miaka mitatu kupata kiungo kinachowafaa.
Wengi ya wagonjwa hao hufariki kabla ya kiungo kupatikana.
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment