Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Wednesday 25 March 2015

WANAWAKE WATANO WAJIANDAA KUWANIA URAIS


Wakati joto la mbio za kuwania urais likiendelea kuisisimua nchi, Umoja wa Wanawake Wanasiasa Tanzania (Ulingo), kwa kushirikiana na Mtandao wa Wanawake na Katiba, umesema tayari wameandaa majina matano ya wanawake kuwania nafasi hiyo baadaye mwaka huu.
Mwenyekiti wa Ulingo, Anna Abdallah bila kutaja majina ya wagombea hao wanawake, alisema jana kuwa waliopendekezwa, baadhi wanatoka nje ya vyama vya siasa.
Hata hivyo, ingawa hakutaja majina ya wateule hao, wadadisi wa mambo ya siasa wanalitaja jina la Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Asha-Rose Migiro kuwa miongoni.
Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk Hellen Bisimba alisema wameanzaa kampeni hizo tangu Septemba mwaka jana kupitia mradi wa ‘Wanawake na Uchaguzi’.
“Tumeshazunguka mikoa 15 nchini kutoa elimu kwa wananchi kuunga mkono harakati za wanawake katika Uchaguzi Mkuu,” alisema Bisimba.
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Lihundi alisema ataunga mkono jitihada za wanawake kuwania nafasi za uongozi na atafanya hivyo bila kujali itikadi za vyama.
Hadi sasa tayari wanasiasa kadhaa wameonyesha nia ya kuwania nafasi hiyo ya ukuu wa nchi. Miongoni mwao ni Bernard Membe, Edward Lowassa, Khamis Kigwangalla, Januari Makamba, Samuel Sitta, Frederick Sumaye, Stephen Wasira na Mwigulu Nchemba wote kutoka CCM.
Mwenyekiti wa Kigoda cha Taaluma cha Mwalimu Nyerere, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Penina Mlama alisema Tanzania haitakuwa nchi ya kwanza kuingia kwenye mabadiliko ya kuongozwa na mwanamke. “Kuna nchi kama Liberia na Brazil, hizi zinaongozwa na marais wanawake na wanafanya vizuri. Sisi pia tuna wanawake wenye uwezo wa kuongoza, sioni shaka yoyote.”
CREDIT: MWANANCHI

No comments:

Post a Comment