Na George Binagi-GB Pazzo @BMG
Watendaji wa Mahakama nchini wamehimizwa
kufanya kazi kwa uwazi na uadilifu, ili kurejesha imani kwa wananchi juu ya chombo
hicho muhimu katika utoaji wa maamuzi.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella,
alitoa kauli hiyo jana kwenye Mkutano wa robo mwaka wa Chama cha Majaji na Mahakimu
JMAT, tawi la Mwanza na Geita uliofanyika Jijini Mwanza.
Mongella alisema watendaji wa mahakama
wakiwemo Majaji na Mahakimu wanapaswa kutenda haki katika shughuli zao na kuhakikisha
mchango wa mahakama katika utoaji wa haki unaonekana kwa wananchi.
Mwenyekiti wa Chama cha Majaji na
Mahakimu tawi la Mwanza, Francis Kishenyi, ambaye pia ni Hakimu Mkazi Mfawidhi
Wilaya ya Ukerewe, alisema miongoni mwa malengo ya chama hicho ni kuhakikisha watumishi
wa mahakama wakiwemo Majaji na Mahakimu wanafanya kazi kwa kuzingatia maadili
ya mahakama.
Pamoja na mambo mengine, mkutano huo
umejadili masuala mbalimbali ikiwemo maadili ya viongozi wa Umma katika kuwatumikia
wananchi.
Bonyeza HAPA Kutazama Picha
No comments:
Post a Comment