Mkuu wa Wilaya ya Bukoba (DC) Deodatus Kinawiro (wa
kwanza kushoto) akitembelea maeneo mbalimbali katika Chuo cha Ualimu cha Bukoba
kinachomikiwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (BLTC)
kinachomolikiwa na Dayosisi ya Kaskazini Magharibi ambapo wanafunzi wa kidato
cha tano kutoka shule ya sekondari Ihungo wataenda kusoma wakati shule yao
inajengwa upya baada ya kuharibiwa kwa tetemeko la ardhi lililotokea Septemba
10, mwaka huu. Wa kwanza kulia ni Mkufunzi katika chuo hicho Dafroza Protas.
Mkuu wa Wilaya ya Bukoba
(DC) Deodatus Kinawiro (wa kwanza kushoto) akitembelea maeneo mbalimbali katika
Chuo cha Ualimu cha Bukoba kinachomikiwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri
Tanzania (BLTC) kinachomolikiwa na Dayosisi ya Kaskazini Magharibi ambapo
wanafunzi wa kidato cha tano kutoka shule ya sekondari Ihungo wataenda kusoma
wakati shule yao inajengwa upya baada ya kuharibiwa kwa tetemeko la ardhi
lililotokea Septemba 10, mwaka huu. Wa kwanza kulia ni Mkufunzi katika chuo
hicho Dafroza Protas.
Mkuu wa Wilaya ya Bukoba (DC) Deodatus Kinawiro (wa pili
kushoto) akikagua moja ya matanki ya kuhifadhia maji katika Chuo cha Ualimu cha
Bukoba kinachomikiwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (BLTC) cha
Dayosisi ya Kaskazini Magharibi ambapo wanafunzi wa kidato cha tano kutoka
shule ya sekondari Ihungo wamehamishiwa kusoma wakati shule yao inajengwa upya
baada ya kuharibiwa kwa tetemeko la ardhi lililotokea Septemba 10, mwaka huu.
Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bukoba Mwantum Dau.
06. Muonekano wa baadhi ya majengo yatakayotumiwa na wanafunzi
wa kidato cha tano kutoka shule ya sekondari Ihungo wataenda kusoma wakati
shule yao inajengwa upya baada ya kuharibiwa kwa tetemeko la ardhi lililotokea
Septemba 10, mwaka huu.
(Picha na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Bukoba)
Na Eleuteri Mangi,
MAELEZO, Bukoba
Serikali
imesema shule wanapohamishiwa wanafunzi wa kidato cha tano na cha sita baada ya
shule za sekondari za Ihungo na Nyakato kuharibiwa na tetemeko la ardhi
kuharibu miundombinu ya shule hizo Septemba 10 mwaka huu.
Akizungumzia
miundombinu ya Chuo cha Ualimu cha Bukoba kinachomikiwa na Kanisa la Kiinjili
la Kilutheri Tanzania (BLTC) kinachomolikiwa na Dayosisi ya Kaskazini Magharibi
alipotembelea chuoni hapo, Mkuu wa Wilaya ya Bukoba (DC) Deodatus Kinawiro
amesema kuwa mazingira wanapohamishiwa wanafunzi wa kidato cha tano kutoka
shule ya sekondari Ihungo ni mazuri kwa kusomea yatawasaidia kupata elimu kama
walivyokuwa kwenye shule yao ya Ihungo.
“Mazingira
ya chuo ni mazuri sana, Serikali inaendelea kufanya marekebisho madogo madogo
maeneo mbalimbali ya chuo ikiwa ni pamoja na miundombinu ya maji ili wanafunzi
waendelee na masomo bila adha yeyote itakayowakwamisha kupata elimu” alisema DC Kinawiro.
DC
Kinawiro ameongeza kuwa Serikali imechukua hatua za haraka za kunusuru athari
ambazo zingeweza kuwapata wanafunzi ambao shule zao zimeathirika zaidi kwa
tetemeko la ardhi ambapo imelazimu kuwahamishia wanafunzi hao shule nyingi huku
shule zao za awali za Ihungo na Nyakato zikiwendelea kujengwa upya.
Kuhusu
kuwasili wanafunzi wa kidato cha tano katika chuo cha ualimu cha BLTC mwishoni mwa wiki hii, Mkuu
huyo wa wilaya amesema kuwa walimu na wanafunzi hao wafike kwa wakati ili
kuendelea na ratiba ya masomo bila kuchelewa hatua ambayo haitaathiri mtiririko
wa kujifunza na kufundisha.
Akizungumzia
mgawanyo wa wanafunzi wa shule za Ihungo na Nyakato, Afisa Elimu wa Mkoa wa
Kagera Aloyce Kamamba amesema kuwa shule wanapohamishiwa wanafunzi wa shule
hizo mbili zipo tayari kuwapokea wanafunzi hao na walimu wao ili waendelee na
masomo.
Kuhusu
mgawanyo wa wanafunzi katika shule walizopangiwa, Afisa Elimu Kamamba amesema
kuwa wanafunzi wote wa kidato cha sita katika shule za Ihungo na Nyakato wamehamishiwa
katika shule ya sekondari ya Omumwani ambapo wataendelea na masomo yao.
Shule
hiyo ipo manispaa ya Bukoba mjini na miundombinu ya shule hiyo inaruhusu
wanafunzi wa kidato cha sita kuendelea na ikizingatiwa wapo darasa la mtihani
wa taifa ambao kwao ni muda wa maandalizi ya mitihani pamoja na kusoma kwa
vitendo.
Kwa
upande wa wanafunzi wa kidato cha tano kutoka shule ya sekondari Nyakato, Afisa
Elimu Kamamba amesema kuwa wanafunzi wanaosoma tahasusi ya PCM ambao idadi yao
ni 75 wamehamishiwa katika shule ya sekondari Kahororo, PGM wanafunzi 65
wamehamishiwa shule ya sekondari Biharamulo, CBG wanafunzi 95 wamehamishiwa shule ya
sekondari Nyailigamba, HKL wanafunzi 30 wamehamishiwa shule ya sekondari
Kishoju, HGK wanafunzi 30 wamehamishiwa shule ya sekondari Nyakahura na HGE wanafunzi
45 wamehamishiwa shule ya sekondari Nyakahura.
Aidha,
Afisa Elimu amewataka walimu na wanafunzi kitunza miundombinu ya shule
wanazohamishiwa ili iendelee kuwasaidia wanafunzi katika kizazi cha sasa na
kizazi kijacho na kuwahimiza walimu kutimiza wajibu wao wa kuwalea wanafunzi
kitaaluma na kijamii kwa kuwa hiyo ndio kazi waliosomea.
No comments:
Post a Comment