Na Georgina Misama-MAELEZO
Serikali
imesema asilimia 90 ya maoni yaliyotolewa na wadau mbalimbali wa sekta
ya habari nchini yanaohusu Muswada wa Huduma ya Habari wa mwaka 2016
yamechukuliwa na kujumuishwa kwenye muswada huo.
Hayo
yamesemwa leo na Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO ambaye pia ni
msemaji wa serikali Bwn Hassan Abbas wakati wa kipindi cha TUONGEE
ASUBUHI kinachorushwa na kituo cha televisheni cha Star Tv kuhusu Muswada wa Huduma ya Habari.
Bw.
Abbas alisema kuwa moja kati ya jambo la msingi ambalo serikali
iliyafanya wakati wa uandaaji wa muswada huo ni kuwakutanisha na
kuwashirikisha wadau wa sekta ya habari kutoa maoni ili kuuboresha na
kwa kuzingatia umuhimu ya maoni waliyoyatoa kwa kiasi kikubwa serikali
imeyajumuisha kwenye muswada huo.
“Vitu
ambavyo serikali isingeweza kuvipuuza ni maoni ya wadau wa sekta ya
habari kuhusu muswada huu na nikuhakikishie kuwa asilimia 90 ya maoni
yaliyotolewa na wadau yamejumuishwa na lengo ni moja tu kuja na sheria
nzuri itakayoiongoza sekta ya habari na hatimaye kuiwezesha sekta hii
iheshimike na iwe rasmi” alisema Bw Abbas
Aidha,
Mkurugenzi Abbas alisema kuwa sekta ya habari ni sawa na sekta nyingine
yeyote nchini, ina haki na wajibu wake na kuwashauri wadau kuangalia
zaidi upande wa haki zao
zitakazopatikana kwenye mswada huo badala ya kulalamika ili kwa pamoja
waweze kulivusha suala hili kwa ustawi wa sekta ya habari nchini.
Wakatihuo
huo Bw. Abbas amewataka wadau wa sekta ya habari nchini kuendelea
kujenga hoja hasa kwenye maeneo wanayotaka kuboreshwa kwenye muswada huu
ili kuisaidia taaluma ya habari kukua na kuheshimika kama fani nyingine
nchini.
No comments:
Post a Comment