Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan (kulia) akiagana na mgeni wake Makamu wa Rais wa Cuba Mhe.
Salvador Antonio Valdes Mesa ambaye amemaliza ziara ya siku 3 ya kikazi
nchini.
............................................................
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Cuba Salvador Antonio Valdes Mesa ameondoka nchini mchana
huu baada ya kumaliza ziara ya kiazi ya siku tatu kwa mwaliko wa Makamu wa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.
Lengo la
ziara hiyo ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Cuba Salvador Antonio Valdes Mesa ni
kuendeleza na kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Cuba hasa katika sekta
mbalimbali ikiwemo elimu,afya,utamaduni,michezo na utalii.
Katika sekta ya utalii, Serikali
ya Cuba imeahidi kuisaidia Tanzania
katika kuendeleza utalii katika fukwe pamoja na kubadilishana uzoefu na
wataalamu wa hapa nchini katika sekta hiyo ili kusaidia kuongeza pato la taifa
kupitia shughuli za utalii nchini.
Aidha
kwenye sekta ya viwanda Tanzania na Cuba zimekubaliana kushirikiana katika
ujenzi wa kiwanda cha kisasa cha kutengenezea madawa ya binadamu nchini.
Katika
uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Cuba Salvador Antonio Valdes Mesa ameagwa na mwenyeji wake Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan baada ya kuhitimisha ziara yake
nchini.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan (kulia) akimsindikiza mgeni wake Makamu wa Rais wa Cuba Mhe.
Salvador Antonio Valdes Mesa ambaye amemaliza ziara ya siku 3 ya kikazi
nchini.
No comments:
Post a Comment