Mkuu wa Wilaya Bukoba Deodatus Kinawiro
akiwashukuru Taasisi ya Kimataifa ya Lions Club ya jijini Mwanza kwa niaba ya
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Salum Kijuu na kusema kuwa mahitaji kwa
waathirika wa tetemeko la ardhi bado ni makubwa na misaada inahitajika ili
kuwasaida waathirika hao.
Mratibu Mkuu wa Taasisi ya Kimataifa ya Lions Club ya jijini Mwanza Burhan
Mohammed akitoa neno mwishoni mwa wiki mara baada ya ya kukabidhi msaada wa
vyakula kuwasaidia wakazi wa mkoa wa Kagera ambao wameathiriwa na tetemeko la
ardhi mapema mwezi Septemba mwaka huu.
Mkuu wa Wilaya Bukoba Deodatus Kinawiro (katikati aliyevaa suti) akiwa katika
picha ya pamoja na wanachama wa Taasisi ya Kimataifa ya Lions Club ya jijini
Mwanza mara baada ya kukabidhi msaada wa vyakula kuwasaidia wakazi wa mkoa wa
Kagera ambao wameathiriwa na tetemeko la ardhi mapema mwezi Septemba mwaka huu.
(Picha
na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Bukoba)
Na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Bukoba
Kamati
ya maafa mkoani Kagera imeendelea kupokea misaada kutoka kwa wadau mbalimbali
wa ndani na nje ya nchi kutoa michango yao kwa lengo la kusaidia waathirika wa
tetemeko la ardhi lililoathiri mkoa wa Kagera.
Akikabidhi
msaada uliotolewa na Taasisi ya Kimataifa ya Lions Club ya jijini Mwanza
Mratibu Mkuu wa taasisi hiyo Bw. Burhan Mohammed amesema kuwa wao kama taasisi
wamevutwa na kushikwa kwa moyo wa huruma na kuamua kuchukua hatua ya kuwasidia
majirani zao wa mkoa wa Kagera.
Sisi
sote ni Watanzania, tuliposikia wenzetu wamepatwa na matatizo, tumeamua kutoa
mchango wetu kwa kushirikiana na wanachama wenzetu ili kutoa huduma za kuwapa
chakula wenzetu wakati wa matatizo” alisema.
Taasisi
hiyo imetoa Mchele, chumvi, mafuta ya kula, Sabuni pamoja na katoni za maji ya
kunywa ambapo vyote kwa jumla vinathamani ya sh. milioni 22.
Aidha,
Kanisa la Anglikana Tanzania Dayosisi ya Lwelu ya mkoani Kagera wametoa
vyakula vyenye thamani ya shilingi milioni 2.1 ikiwa ni pamoja na sukari, unga
na mchele.
Wadau
wengine waliotoa misaada ni kampuni ya Time to Help yenye makao makuu ya jijini
Dar es salama ambayo inayomilikiwa Waturuki wametoa mablanket 500.
Akipokea
misaada hiyo kwa niaba ya Mkuu Mkoa wa Kagera, Mkuu wa Wilaya Bukoba Deodatus Kinawiro
amewaeleza wadau hao taswira mzima ya hali ya maafa katika mkoa Kagera ambapo
amesema kuwa mahitaji kwa waathirika bado ni makubwa.
Kwa
niaba ya Serikali, Mkuu wa Wilaya Bw. Kinawiro amewashukuru wadau wote
wanaendelea kutoa misaada kwa lengo la kuwasaidia wananchi wa Kagera ambao
wameathirika wa tetemeko hilo na kuwataka wadau wengine kuendelea michango ya
hali na mali katika kukabiliana na hali ya maisha baada ya tetemeko kutokea.
No comments:
Post a Comment