Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akihutubia kwenye mkutano wa kwanza wa Wafanyabiashara wa
Tanzania na Morocco utakaoainisha fursa za uwekezaji baina ya nchi hizo
mbili uliofanyika kwenye Hotel ya Hyatt Regency.
Wafanyabiashara wa
Tanzania na Morocco wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan alipokuwa akihutubia kwenye mkutano wa Kwanza wa Wafanyabiashara wa
Tanzania na Morocco utakaoainisha fursa za uwekezaji baina ya nchi hizo
mbili uliofanyika kwenye Hotel ya Hyatt Regency.
Katika Hotuba yake ya ufunguzi wa Mkutano wa kwanza wa
wafanyabiashara na Wawekezaji wa Tanzania na Morocco Makamu wa Rais aliainisha maeneo mbali
mbali ambayo yanaweza kuwa fursa nzuri ya kuwekeza Tanzania.
Baadhi ya maeneo hayo ni Kilimo,Utalii, Nishati, Mafuta na
Gesi, Viwanda,Sekta ya Huduma, na Sekta ya Madini
Mbali na kuainisha
baadhi ya fursa Makamu wa Rais aliwahakikishia uwepo wa amani na usalama na sheria mbalimbali zinazolinda haki za wawekezaji.
Rais wa Chama cha Wafanyabiashara wa Morocco Bi.Miriem Bensalah-Chaqroun, akihutubia kwenye mkutano wa kwanza wa Biashara na Uwekezaji baina ya Tanzania na Morocco uliofanyika kwenye Hotel ya Hyatt Regency.
Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage akizungumza wakati wa mkutano wa kwanza uliowakutanisha wafanyabiashara wa Tanzania na Morroco.
Sehemu ya wafanyabiashara kutoka Morocco wakifuatilia kwa makini mkutano huo.
No comments:
Post a Comment