Meneja wa mauzo wa Sbl Mkoani Kilimanjaro Godwin Seleliii akizungumza katika mkutano na wadau kuhusu kampeni ya unywaji kistaarabu iliyofanyika katika mji wa Moshi mkoani kilimanjaro mapema jana. |
Mkaguzi wa polisi Mkoa wa kilimanjaro Peter Mizambwa akitoa hotuba kwa wageni waliohudhuria uzinduzi wa keampeni ya unywaji kistarabu iliyozinduliwa mapema jana na Sbl katika mji wa Moshi |
Wadau mbalimbali wakifuatilia kwa makini elimu juu ya unywaji wa kistaarabu katika uzinduzi wa kampeni hiyo mapema jana |
Waendesha bodaboda wakipata elimu ya unywaji kistaarabu kutoka kwa mfanyakazi wa SBL aliyekuwa anapita mitaani |
Mdau akiwa na zawadi ya kava la gari mara baada ya kujibu vizuri maswali yaliyoulizwa kuhusu unywaji wa pombe kistaarabu |
Moshi, Oktoba 18, 2016. Kampuni ya bia ya Serengeti imezindua kampeni inayohamasisha matumizi sahihi ya pombe au unywaji pombe kistaarabu. Kampeni hii ni hatua muhimu katika sekta ya biashara ya pombe kwa kutambua changamoto inazokabiliana nazo hususan katika masuala ya uwajibikaji kwa jamii.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo Mkaguzi wa polisi Mkoa wa Kilimanjario, Peter Mizambwa , amesema kulishirikisha jeshi la polisi, kikosi cha usalama barabarani, kunaonyesha ni kwa jinsi gani SBL wanatilia maanani suala zima la usalama barabarani hasa matokeo ya ulevi na uendeshaji vyombo vya moto. Uzoefu unaonyesha kwamba watu wengi hujisahau na kujiingiza katika ulevi wa kupindukia bila kuzingati vyombo vya moto wanavyoendesha.
“Ni jambo lilisilopingika kuwa uzembe na unywaji wa pombe kupita kiasi vina athari kubwa kwa jamii. Madhara hayo hayamuathiri mtumiaji wa pombe peke yake, bali uhatarisha maisha na kuathiri mustakabali wa watu wengi” aliongeza Mizambwa .
“Kwa matinki hiyo, ni janga la jamii nzima – huduma zetu za afya zimeelemewa kwa kiasi kikubwa na wale waliojeruhiwa katika masuala yanayohusiana na ajali na uhalifu; taasisi zetu za masuala ya sheria zimeelemewa vilivyo; uzalishaji unaathirika mno na kwa mlolongo huo, ukuaji wa pato la taifa hubakia kuwa wa kiwango cha chini”, alisema Bi Zauda.
Akielezea jinsi kampeni hii itakavyosaidia Mizambwa anasema “ma kwa hakika, sote kwa ujumla wetu tunaathirika – na sote tunalo jukumu la kuchangia namna bora ya kukabiliana na tatizo la ulevi. Nafurahi kuona kwamba wazalishaji wenyewe wa vinywaji vya pombe wametambua kuwa biashara wanayofanya kwa wateja wao inahitaji uwajibikaji na umakini wakati wa kutumia”.
Kampeni hii ya unywaji wa kistaarabu inakusudia kuwafikia vijana wengi pamoja na watu wa rika la juu kwa kuwataka kuelewa hatari ya matumizi ya pombe na kufanya maamuzi kwa faida zao – maamuzi ambayo yatanusuru mustakabali wao wa baadaye.
Naye Meneja wa SBL wa Uwajibikaji Katika Jamii, Hawa Ladha, amesema kampeni ya unywaji pombe kistaarabu inalenga kuwapa walengwa elimu kwamba mtumiaji wa pombe hahitaji kutawaliwa na pombe na kuipa nafasi ibadili mustakabali wa maisha wake na kuongeza kwamba vifo na ajali nyingi hutokana na uzembe au ulevi wa watu ambao si waathirika wakubwa wa pombe – ambao wangeweza kuwa waangalifu kama wangechukua tahadhari na kujifikiria marambili au kama marafiki zao wasingewahamasisha ku-“ongeza moja …au mbili”, alisema.
No comments:
Post a Comment