Mwenyekiti
wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani
ambaye pia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi
Hamad Masauni, akizungumza na wajumbe wa baraza hilo wakati wa kikao cha
kujadili maendeleo ya Mkakati wa Kupunguza Ajali za Barabarani. Kulia ni Katibu
Mtendaji wa baraza ambaye pia ni Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani,
Mohamed Mpinga.Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa wizara hiyo, Dar es
Salaam. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).
Katibu
Mtendaji wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani nchini ambaye pia ni Kamanda wa Kikosi cha Usalama
Barabarani, Mohamed Mpinga, akifungua kikao cha kujadili maendeleo ya Mkakati
wa Kupunguza Ajali za Barabarani. Kushoto ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama
Barabarani ambaye pia ni Naibu Waziri wa
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni. Kikao hicho
kimefanyika katika ukumbi wa wizara hiyo, Dar es Salaam. (Picha na Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi)
Mwenyekiti
wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani
ambaye pia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi
Hamad Masauni, akiongoza kikao cha kujadili maendeleo ya Mkakati wa Kupunguza
Ajali za Barabarani. Kushoto ni Katibu
Mtendaji wa baraza ambaye pia ni Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani
nchini, Mohamed Mpinga.Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa wizara hiyo,
Dar es Salaam. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
Mjumbe
wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani kutoka Kikosi cha Usalama Barabarani, Mrakibu
Msaidizi wa Jeshi la Polisi, Mossi Ndozero, akiwasilisha taarifa ya maendeleo
ya Mkakati wa Kupunguza Ajali za Barabarani kwa Mwenyekiti wa Baraza la Taifa
la Usalama Barabarani ambaye pia ni
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(hayupo
pichani), wakati wa kikao cha kujadili maendeleo ya mkakati huo, kilichofanyika
katika ukumbi wa wizara, Dar es Salaam. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi)
Mjumbe
wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Hamza Kasongo(kulia), akichangia mada
wakati wa kujadili taarifa ya maendeleo
ya Mkakati wa Kupunguza Ajali za Barabarani wakati wa kikao cha kujadili
maendeleo ya mkakati huo.Kushoto ni mjumbe wa baraza hilo Henry Bantu. Kikao
hicho kilifanyika katika ukumbi wa
wizara, Dar es Salaam.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
IMEANDALIWA
NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI, WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.
No comments:
Post a Comment