Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.
Dkt. John Pombe Magufuli akizindua mitambo inayojenga daraja la waenda kwa
miguu na upanuzi wa Barabara ya Uwanja wa Ndege eneo la Furahisha jijini
Mwanza, wa pili kutoka kulia ni Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli na watatu
kutoka kulia ni Naibu Waziri wa Ujenzi Eng. Edwin Ngonyani.
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Eng. Joseph Nyamhanga kulia akijadiliana jambo na
Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Barabara (RFB), Bw. Joseph Haule katikati na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa barabara nchini
Eng. Patrick Mfugale wa kwanza kushoto katika hafla ya uzinduzi wa daraja la
watembea kwa miguu lililopo maeneo ya Furahisha jijini Mwanza.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa barabara nchini
Eng. Patrick Mfugale akimuonesha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.
Dkt. John Pombe Magufuli wa tatu kulia michoro ya muonekano wa daraja la waenda
kwa miguu na upanuzi wa Barabara ya Uwanja wa Ndege eneo la Furahisha jijini
Mwanza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.
Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na wafanyakazi wa kampuni ya Nyanza Road Works
inayojenga daraja la waenda kwa miguu na upanuzi wa Barabara ya Uwanja wa Ndege
eneo la Furahisha jijini Mwanza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.
Dkt. John Pombe Magufuli akipata ufafanuzi wa maendeleo ya ujenzi wa daraja la
waenda kwa miguu na upanuzi wa Barabara ya Uwanja wa Ndege eneo la Furahisha
jijini Mwanza kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa barabara nchini Eng.
Patrick Mfugale. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Bw. John Mongela.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.
Dkt. John Pombe Magufuli akihitubia wananchi katika mkutano wa hadhara mara
baada ya uzinduzi wa daraja la watembea kwa miguu na upanuzi wa Barabara ya
Uwanja wa Ndege eneo la Furahisha jijini Mwanza.
Sehemu ya wananchi wakimsikiliza Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. John Pombe Magufuli alipohutubia
mkutano wa hadhara katika uwanja wa Furahisha jijini Mwanza. (PICHA ZOTE NA
BENJAMIN SAWE-MAELEZO)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.
Dkt. John Pombe Magufuli ameitaka Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano kuhakikisha
kuwa ujenzi wa daraja la watembea kwa miguu na upanuzi wa Barabara ya Makongoro
jijini Mwanza unakamilika ifikapo disemba mwaka huu.
Aidha amesema upanuzi wa barabara ya Makongoro
uliokuwa ujengwe kati ya Furahisha hadi Pasiansi Km 2.8 sasa utaendelezwa hadi
kufikia uwanja wa ndege.
Akizungumza mara baada ya kuweka jiwe la
msingi la daraja la watembea kwa miguu na upanuzi wa barabara ya Makongoro Mh.
Dkt. Magufuli amesema kasi ya ujenzi wa barabara jijini Mwanza uendane na
ujenzi wa uwanja wa ndege ili kuwezesha mkoa wa Mwanza kuwa kitovu cha nchi za
maziwa makuu.
“Nakuagiza Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na
Mawasiliano uhakikishe kuwa barabara na
daraja la watembea kwa miguu Furahisha vinakamilika mwezi desemba na mkandarasi
wa uwanja wa ndege anaanza kazi mara moja”. Amesisitiza Rais Dkt. Magufuli.
Amesema nia ya Serikali yake ni kununua
meli mbili na kujenga daraja kati ya Kigongo na Busisi ili kuboresha huduma za
usafiri katika Ziwa Victoria.
Naye Mtendaji mkuu wa Wakala wa Barabara
Tanzania (TANROADS), Eng. Patrick Mfugale amemtaka mkandarasi anaejenga daraja
la waenda kwa miguu na barabara ya Makongoro kuhakikisha ujenzi wake
unakamilika kwa wakati na ubora unaotakiwa.
Zaidi ya shilingi bilioni 6.4 zinatarajiwa
kutumika katika ujenzi huo utakaopunguza msongamano wa magari na ajali katika
barabara ya makongoro jijini Mwanza.
IMETOLEWA
NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA
MAWASILIANO.
No comments:
Post a Comment