Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini, Ester Bulaya
Na Immaculate
Makilika- MAELEZO
Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Jimbo la Bunda Bi. Janet Mayanja amepokea madawati 90
yalitolewa na Mbunge wa Jimbo hilo kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA) Bi. Ester Bulaya, ambapo hapo awali madiwani
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika jimbo hilo walikataa kupokea madawati hayo
baada ya kuwa yameandikwa jina la
mbunge huyo pamoja na kuwa yamenunuliwa na fedha za Mfuko wa Jimbo.
Akizungumza
leo kwa njia ya simu, Mkurugenzi Mayanja
alisema kuwa amepokea madawati
hayo Agosti 12 kutoka kwa Mbunge wa jimbo hilo Ester Bulaya baada ya
kufutwa jina lake, ambapo madawati hayo tayari yamewasilishwa katika shule tatu
zilizokuwa na uhaba.
“Tulifanya
kikao na Mbunge Bulaya na tukakubaliana kuwa ni vyema majina yake yakafutwa
katika madawati hayo kwa vile yalinunuliwa kwa fedha za Mfuko wa Jimbo, lakini endapo mbunge
atapenda kutupa madawati atakayonunua kwa fedha
zake binafsi na kuandika majina
yake hapo tutapokea kwa vile bado kuna tunauhitaji katika jimbo letu,” alisema
Mkurugenzi Mayanja.
Alifafanua
kuwa fedha zilizotumika kununua madawati hayo zilikuwa ni fedha za Mfuko wa Jimbo zinazotokana na ruzuku ya
Serikali ambazo matumizi yake hupangwa na Ofisi ya Mbunge.
Madawati hayo
90 yalisambazwa katika shule tatu za Msingi zilizopo katika Jimbo la Bunda
zilizokuwa na uhaba wa madawati ambazo
ni Nyatwali, Nyerere na
Ligamba, zilizopewa
madawati 30 kwa kila moja.
No comments:
Post a Comment