Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka akizungumza na Wakuu wa Wilaya, Makatibu
Tawala Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri za
Mkoa huo (hawapo pichani), katika Mafunzo elekezi yaliyotolewa kwa
viongozi hao Mjini Bariadi kwa lengo la kuwajengea uwezo wa Kiutendaji.
Katibu
Tawala Mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini(kushoto) akitoa maelezo ya utangulizi kwa Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala
Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa huo (hawapo pichani) kabla ya
kumkaribisha Mkuu wa Mkoa huo Anthony Mtaka (kulia) kufungua Mafunzo elekezi
kwa viongozi hao
Baadhi
ya Wajumbe wakimsikiliza Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka (hayupo pichani) wakati akifungua mafunzo elekezi
kwa Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri
za Mkoa huo, yaliyotolewa kwa lengo la
kuwajengea uwezo wa Kiutendaji.Mstari wa Kwanza kutoka kushoto Wakuu wa
Wilaya,Tano Mwera (Busega), Seif Shekalaghe (Maswa), Joseph Chilongani (Meatu),
Benson Kilangi (Itilima) na Festo Kiswaga (Bariadi).
Wakuu
wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Simiyu wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka
(hayupo pichani) wakati akifungua mafunzo elekezi kwa Wakuu wa Wilaya, Makatibu
Tawala Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri za
Mkoa huo, yaliyotolewa kwa lengo la kuwajengea uwezo wa Kiutendaji.
Kutoka (kushoto) Kamanda wa Polisi Mkoa, Mkuu wa Usalama wa Taifa, Afisa
Uhamiaji, Kamanda wa Zimamoto na Mkuu wa TAKUKURU
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka (wa pili kulia kwa waliokaa) akiwa katika
picha ya pamoja na Wakuu wa Vyombo Vya
Ulinzi na Usalama Mkoa, Makatibu Tawala Wasaidizi, Wakuu wa Wilaya, Makatibu
Tawala Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri za
Mkoa huo, baada ya kufungua Mafunzo elekezi yaliyotolewa kwa viongozi
hao wa Wilaya Mjini Bariadi, kwa lengo la kuwajengea uwezo wa Kiutendaji. (wa
pili kushoto)Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini (kushoto)Mkuu wa
Wilaya Busega, Tano Mwera na( kulia) Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Festo Kiswaga.
Na Stella Kalinga, SIMIYU
Serikali Mkoani
Simiyu imesema haiko tayari kuwavumilia na kuwaacha katika vyeo na majukumu
waliyonayo watendaji wanaotoa takwimu zisizo za kweli.
Kauli hiyo
imetolewa na Mkuu wa mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka wakati wa ufunguzi wa mafunzo
elekezi yaliyotolewa kwa Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala Wilaya na Wakurugenzi
wa Halmashauri za Mkoa huo, yaliyofanyika jana Mjini Bariadi, kwa lengo la
kuwajengea uwezo wa kiutendaji, kwa kuwa baadhi ya viongozi hao wametoka katika
sekta binafsi ambazo zina mifumo tofauti ya kitendaji na mfumo wa Serikali.
“Tunawezaje
kukaa na Mtendaji ambaye ukimwomba taarifa za upungufu wa madawati anadanganya,
idadi ya wanafunzi anadanganya, walimu anadaganya tutamchukulia hatua tu.
Lazima tupeleke ujumbe kwamba taarifa za uongo hazina nafasi tena katika Mkoa
wa Simiyu. Namwagiza Katibu Tawala Mkoa, aanze kuchukua hatua stahiki dhidi ya
watendaji wote waliotoa taarifa zisizo za kweli hususani katika takwimu za wanafunzi, walimu,
madawati na vyumba vya madarasa”, alisema Mtaka.
Mtaka amesema
azma ya Serikali Mkoani humo ni kuhakikisha Nafasi za watendaji wasio waadlifu
zinajazwa na watumishi waadilifu, wenye sifa na elimu ya kutosha waliopo katika
Halmashauri za Mkoa huo.
Aidha, Mkuu huyo
wa Mkoa amewataka viongozi hao wa Wilaya kubaini watumishi wenye sifa na uwezo
wa kutekeleza majukumu ya Serikali katika maeneo yao na wawape fursa watumie
talanta zao kwa manufaa ya wananchi na Taifa kwa ujumla.
Pamoja na
kubaini watumishi wenye sifa, viongozi hao wameelekezwa kuwachukulia hatua
watumishi wanaopenda kufanya kazi kwa mazoea, ikiwa ni pamoja na kuwapangia
majukumu yanayoendana na uwezo wao wa kufanya kazi.
Katika kuboresha
ukusanyaji wa mapato, Mtaka ametoa wito kwa viongozi hao kuibua vyanzo vipya
vya mapato na kusimamia ukusanyaji wa Mapato hayo kwa kuzingatia maagizo ya
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ya
kutowabugudhi wananchi wanyonge na akawataka Wakurugenzi wa Halmashauri kuhakikisha wanatenga asilimia 10 ya mapato
yao ya ndani kwa ajili ya kuimarisha vikundi vya uzalishaji vya vijana na
wanawake
Sanjari na hilo Mtaka
amewataka Viongozi hao wa Wilaya kutambua fursa za maendeleo katika maeneo yao
na kuzitekelezafursa hizo kwa manufaa ya Wananchi walio katika maeneo yao.
Akizungumza
baada ya mafunzo hayo, Mkuu wa Wilaya ya Busega Mhe, Tano Mwera alisema mafunzo
hayo yamemsaidia kumpa mwanga na dira ya
utendaji katika nafasi yake hasa katika utaratibu wa mawasiliano na mahusiano
kati ya Serikali Kuu na Serikali za Mitaa kwa Mujibu wa Sheria, Kanuni na
Taratibu za Nchi, Nafasi yake kama Kiongozi wa Serikali Wilayani pamoja na
Sheria na Miongozo ya Vyombo vya Ulinzi na Usalama.
Mafunzo hayo ya siku
moja kwa Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri ambayo
yaliongozwa na Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini. yaliendeshwa na
Makatibu Tawala Wasaidizi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Wakuu wa Vyombo vya
Ulinzi na Usalama wa Mkoa huo.
No comments:
Post a Comment