Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Monday, 29 August 2016

WAZIRI WA FEDHA AKUTANA NA WAFANYABIASHARA KIGOMA


Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (kushoto) akimsikiliza kwa makini Bi. Rehema Kabuye (katikati) aliyekua akilia kwa uchungu, akimsihi Waziri huyo wa Fedha na Mipango, amsaidie ili mume wake ambaye ni Nahodha wa meli ya MV Liemba pamoja na wafanyakazi wengine wa Mamlaka ya Huduma za meli mkoani Kigoma, walipwe mishahara yao ya miezi nane ili kuwaondolea adha ya maisha inayowakabili wao na familia zao.

Bi. Rehema Kabuye, (Katikati) ambaye ni mke wa Nahodha wa Meli ya Mv Liemba, inayotoa huduma zake Ziwa Tanganyika, akimwonesha Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), picha za mtoto wake ambaye ana matatizo ya kiafya, akimsihi Waziri huyo amsaidie yeye pamoja na wenzake ili waume zao walipwe mishahara yao ya miezi 8 wanayomdai mwajiri wao, Mamlaka ya Huduma za Meli mkoani Kigoma.
Katibu wa Waziri wa Fedha na Mipango, Edwin Makamba (Kulia), akichukua maelezo ya kina kutoka kwa Bi. Rehema Kabuye, Mkazi wa Kigoma, ambaye amemwomba Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), aingilie kati sakata la waume zao wanaofanya kazi kwenye mamlaka ya huduma za meli mkoani Kigoma, ambao hawajalipwa mishahara yao kwa muda mrefu.
Baadhi ya wafanyabiasha wa Kigoma Mjini, wakimsikiliza kwa makini waziri wa fedha na Mipango, Mhe. Dkt Philip Mpango (Mb) (hayupo pichani), wakati wa mkutano na Waziri huyo kuhusu masuala mbalimbali ya biashara na ulipaji kodi, mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa NSSF, mjini Kigoma.
Baadhi ya wafanyabiasha wa Kigoma Mjini, wakimsikiliza kwa makini waziri wa fedha na Mipango, Mhe. Dkt Philip Mpango (Mb), wakati wa mkutano na Waziri huyo kuhusu masuala mbalimbali ya biashara na ulipaji kodi, mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa NSSF, mjini Kigoma.
Baadhi ya maofisa wa Wizara ya Fedha na Mipango, wakifuatilia kwa makini hotuba ya Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), wakati wa mkutano wake na wafanyabiashara wa Kigoma Mjini, mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa NSSF, mjini Kigoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), aliyesimama kushoto, akiwahutubia wafanyabiasha wa Kigoma Mjini, kuhusu masuala mbalimbali ya biashara na ulipaji kodi, mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa NSSF, mjini Kigoma.
Katibu wa Jumuiya ya Wafanyabiashara mkoa wa Kigoma Bw. Raymond Ndabiyegetse (katikati) akichangia hoja katika kikao na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (hayupo pichani) ambaye alipongeza juhudi zinazofanya na Serikali katika kutengeneza mazingira mazuri ya biashara zao.
Mkurugenzi wa kampuni ya Aifola ya Mjini Kigoma, Bw. Zubery Mabie, akiongea kwa hisia kali akishutumu TRA na maafisa wengine wa serikali katika kituo kidogo  cha Forodha cha Manyovu kilichoko mpakani mwa Tanzania na Burundi, kujihusisha na rushwa kwa kupitisha maroli yakiwa na mizigo, ikiwemo chokaa anayozalisha, bila kulipia kodi. Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), ameahidi kulifanyiakazi suala hilo.
Mmoja wa wafanyabiashara wa Mjini Kigoma akichangia hoja katika mkutano ulioitishwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), kuhimiza ulipaji kodi, matumizi adili ya fedha za umma, matumizi ya Mashine za Kieletroniki na utoaji wa risiti,  mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa NSSF, mjini Kigoma.
Askofu Mstaafu wa Kanisa la Anglican, Dkt. Gerard Mpango, akitoa mchango wake wa mawazo ambapo ameitaka serikali kutoa elimu ya kutosha ya biashara na ujasiriamali kwa wafanyabiashara nchini ili waweze kutumia fursa zilizopo katika soko la Afrika Mashariki, kukuza mitaji na biashara zao, wakati wa mkutano wa wafanyabiashara  na Waziri wa fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), hayupo pichani, uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa NSSF, mjini Kigoma
Kamisha Msaidizi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, anayeshughulikia masuala ya kodi, Bw.  Shogholo Msangi akifafanua kuhusu kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwa wafanyabiashara wa Kigoma Mjini wakati wa  mkutano na  Waziri wa  Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (mb).
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dokta Philip Mpango (Mb), akizungumza na wafanyabiashara wa Kigoma Mjini, kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo umuhimu wa kulipa kodi na matumizi ya mashine za kieletroniki pamoja na kuwasisitizia kutoa risiti kwa wateja wao. kushoto kwake ni Kamishna Msaidizi anayeshughulikia masuala ya kodi, Wizara ya Fedha na Mipango, Shogholo Msangi, mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa NSSF, mjini Kigoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), akionesha rundo la makaratasi yaliyoandikwa hoja na kero mbalimbali za wafanyabiashara wa mjini Kigoma, wakati wa mkutano kati yake na wafanyabiashara hao, uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa NSSF, mjini Kigoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Askofu Dkt. Gerard Mpango, baada ya kumalizika kwa mkutano wake na wafanyabiashara wa Mkoa wa Mjini Kigoma, uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa NSSF, mjini Kigoma.
Waziri wa  Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (kushoto) akifurahia jambo pamoja na Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini, Mhe. Zitto Kabwe, wakati wakitoka nje ya ukumbi wa mikutano wa NSSF, ulipofanyika mkutano kati ya Waziri wa Fedha na Mipango na wafanyabiashara wa mjini Kigoma.
Mbunge wa Kigoma Mjini, Mhe. Zitto Kabwe  (kushoto), akisisitiza jambo wakati akizungumza na Waziri wa Fedha na Mipango,Dkt. Philip Mpango (Mb), baada ya kumalizika kwa mkutano kati yake na wafanyabiashara wa mjini Kigoma, uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa NSSF, mjini Kigoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), (kushoto) akipeana mkono na Mbunge wa Kigoma Mjini Mhe. Zitto Kabwe, mara baada ya kumalizika kwa mkutano kati ya Waziri huyo na  wafanyabiashara wa Mkoa wa Kigoma uliofanyika katika ukumbi wa NSSF, mjini Kigoma.


No comments:

Post a Comment