Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Wednesday, 24 August 2016

WAZIRI MWIGULU AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA CHINA NCHINI TANZANIA



Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba(kushoto), akimsikiliza Balozi wa China nchini Tanzania Dkt. Lu Youqing (katikati), wakati wa mazungumzo juu ya  masuala ya ushirikiano katika sekta ya ulinzi na  usalama kati ya Tanzania na China, Kulia ni Msaidizi wa Balozi, Wang Fang. Mazungumzo hayo yalifanyika leo,jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba(katikati), akiangalia vipengele mbalimbali vinavyohusu ushirikiano juu ya masuala ya ulinzi na usalama, wakati wa mazungumzo yaliyomhusisha Balozi wa China nchini Tanzania, Dkt. Lu Youqing(kulia). Kushoto ni Mwakilishi Mkazi wa Jamhuri ya Watu wa China, Lin Zhiyong. Mazungumzo hayo yalifanyika leo,jijini Dar es Salaam.
 Mwakilishi Mkazi wa Jamhuri ya Watu wa China, Lin Zhiyong(kulia), Msaidizi wa Balozi wa China nchini Tanzania, AI Zhuan(katikati) na Katibu wa Balozi, Dong Zhenyu(kushoto), wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba(hayupo pichani), wakati wa mazungumzo juu ya  masuala ya ushirikiano katika sekta ya ulinzi na  usalama kati ya Tanzania na China. Mazungumzo hayo yalifanyika leo, jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba(katikati), akiagana na Mwakilishi Mkazi wa Jamhuri ya Watu wa China, Lin Zhiyong, mara baada ya kumaliza mazungumzo juu ya  masuala ya ushirikiano katika sekta ya ulinzi na  usalama kati ya Tanzania na China. Kulia ni Balozi wa China nchini Tanzania, Dkt. Lu Youqing. Mazungumzo hayo yalifanyika leo, jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba(kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa China nchini Tanzania, Dkt. Lu Youqing, mara baada ya kumaliza mazungumzo juu ya  masuala ya ushirikiano katika sekta ya ulinzi na  usalama kati ya Tanzania na China. Mazungumzo hayo yalifanyika leo, jijini Dar es Salaam.



IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

No comments:

Post a Comment