Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday 25 August 2016

TATIZO LA CHADEMA WANAPIMA HOMA KWA KIGANJA!


Na Daniel Mbega
NILIWAHI kuandika wakati fulani kwamba “UKWELI WA MWANASIASA NI JINA LAKE TU”  lakini wakatokea watu wengi kunikosoa, wakipinga uchambuzi wangu huo na wengine wakinitisha kwa maneno kwa sababu tu nilikuwa nimekisema kile ambacho wao ama wapendwa wao hawakupenda kisemwe hata kama kiko wazi.
Ilikuwa ni wakati wa kampeni za kuelekea uchaguzi mkuu 2015 wakati nilipozichambua kauli za mawaziri wakuu wa zamani – Edward Lowassa na Frederick Sumaye – waliokwenda kutafuta hifadhi Chadema baada ya kuona ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) hawana nafasi ya kwenda Ikulu tena kama wakuu wa nchi.
Nilisema kwamba wanasiasa hao wamefuzu katika sanaa. Bora Lowassa tunajua alisomea sanaa, lakini Sumaye alisomea kilimo!
SOMA ZAIDI HAPA

No comments:

Post a Comment