Mkurugenzi
Mtendaji wa taasisi ya Young Scientists Tanzania (YST), Dk. Gozbert
Kamugisha, akimwelekeza jambo mgeni rasmi Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako, kabla ya kuanza kutembelea
maonyesho ya sayansi ya wanafunzi ambayo yamefanyika kwa mwaka wa tano.
Christina
Godfrey Mongi (aliyetazama kamera), mwanafunzi wa kidato cha sita
katika shule ya sekondari Bwiru Girls ya jijini Mwanza, akiwaelekeza
watu mbalimbali kuhusu utafiti wao juu ya kuweka mazingira bora na
salama ya kujifunzi kwa wanafunzi wenye albinism.
Maonyesho yakiwa yanaendelea.
Mbali
ya maonyesho, wanafunzi pia walipata fursa ya kutengeneza marafiki
wapya kama wanavyoonekana hapa wakijadiliana mambo mbalimbali.
Na Daniel Mbega
WAZIRI wa
Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako, amesema serikali
itaandaa mazingira ya kuwaendeleza watoto na vijana wanajihusisha na ubunifu
katika masomo ya sayansi na kushauri mashindano ya sayansi kwa wanafunzi
yafanyike kila wilaya, mkoa na taifa.
Akizungumza wakati
wa utoaji wa tuzo kwa wanafunzi waliofanya vizuri kwenye Mashindano ya Tano ya
Young Scientists Tanzania 2016 katika Ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere
(JNICC) jijini Dar es Salaam jana, Profesa Ndalichako alisema hatma ya Tanzania
iko mikononi mwa wanasayansi na kwamba vijana hao chipukizi ndio msingi mkubwa
wa kuhimiza ushiriki wa wengi na kuibua vipaji vitakakvyolisaidia taifa.
SOMA ZAIDI
SOMA ZAIDI
No comments:
Post a Comment