Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais,Muungano na Mazingira,January Makamba akifungua warsha ya wadau
wa kuhusu ripoti ya taarufa ya mchango wa Tanzania katika juhudi za
kimataifa za kukabiliana na mabadiliko ya Tabia ya Nchi uliofanyika jana
kwenye ukumbi wa Veta mjini Tanga kulia ni Kaimu Mkurungenzi wa Mazingira kutoka Ofisi
ya Makamu wa Rais anayeshughulikia pia mabadiliko ya tabia ya Nchi,
Richard Muyungi na kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga, Mhandisi
Zena Saidi.
Kaimu Mkurungenzi wa
Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia pia
mabadiliko ya tabia ya Nchi,
Richard Muyungi akizungumza katika warsha hiyo ya siku mbili
inayofanyika kwenye ukumbi wa Veta Mkoani Tanga.
Baadhi ya washiriki wa warsha ya
wadau kuhusu ripoti ya Taarifa ya Mchango wa Tanzania katika Juhudi za
Kimataifa za kukabiliana na mabadiliko ya Tabia ya Nchi katika kikao
kilichofanyika kwenye ukumbi wa Veta Jijini Tanga wakimsikiliwa Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira,January Makamba
alikuwa akifungua mkutano huo
TANZANIA inatarajiwa kutumia
takribani dola mil500 hadi ifikapo mwaka
2030 ili kuweza kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi
yanayoendelea katika maeneo mbalimbali hapa nchi.
Kiasi hicho cha bajeti kinatarajiwa kutumika kwa ajili ya
utekelezaji wa miradi mbalimbali ambayo itasaidia kupunguza juhudi za
kupunguza joto zinazosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano
na Mazingira January Makamba wakati wa ufunguzi wa warsha ya wadau
kuhusu ripoti ya taarifa ya mchango wa Tanzania katika juhudi za
kimataifa za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Aliitaja baadhi ya miradi ambayo itatekelezwa ili kupunguza gesi
joto hapa nchini kuwa ni dampo la mtoni katika Jiji la Dar Es
Salaam,miradi ya nishati jadidifu katika maeneo ya Mbinga,Makete,Njombe
Usa River na Ifakara.
“Miradi hiyo yote inajumla ya megawati tano(5MW) za uzalishaji wa
hewa ukaa ambapo iwapo hatua za haraka hazitaweza kuchukuliwa athari za
kimazingira zinaweza kuendelea kujitokeza”alisema Waziri Makamba.
Ambapo alisema katika kushiriki juhudi za kimataifa za kupunguza
uzalishaji wa gesi joto tayari serikali ya Tanzania imeshaanza kutoa
fursa kwa wadau ya kushughulikia mabadiliko ya tabia nchi .
Makamba alisema kuwa mikakati hiyo kwa sasa imeshaanza kutekelezwa
katika ngazi za mikoa wilaya pamoja na Halimashauri mbalimbali hapa
nchini.
“Juhudi za serikali ni kuhimiza matumizi ya gesi asilia katika
uzalishaji wa nishati ya umeme yanaongezeka ili kuweza kupunguza
matumizi ya vifaa vinavyozalisha hewa ukaa ili kukabiliana na kasi ya
mabadiliko ya tabia nchi”alisisitiza Waziri Makamba.
Kwa upande wake Kaimu Mkurungenzi wa Mazingira kutoka wizarani
Richard Muyungi alisema kuwa sasa wapo kwenye mkakati wa kutoa elimu
kwa wadau wa mazingira kwenye kanda mbalimbali nchini.
Alisema ilikuweza kuwa na mipango madhubuti katika utekelezaji
mkakati wa taifa wa mawasilinao wa mabadiliko ya tabia nchi kupitia
wizara za kisekta.
No comments:
Post a Comment