Tume ya Uchaguzi (NEC) imewaengua
wagombea urais wa vyama vya Ada/Tadea, DP, CCK na AFP leo kwa maelezo
kuwa wamekosa vigezo vya kugombea nafasi hiyo kubwa ya uongozi hapa
nchini.
Kwa mantiki hiyo, Mchungaji Christopher
Mtikila (DP), Godfrey Malissa (CCK) na John Chipaka (Ada-Tadea)
hawatashiriki katika kinyang’anyiro hicho baada ya fomu zao kuonekana
kuwa zina kasoro huku mgombea urais wa AFP, Omari Sombi akiungana na
wanasiasa hao kutogombea baada ya kushindwa kurejesha fomu ya urais.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa NEC, Jaji
Damian Lubuva, wagombea wa vyama vinane kati ya 12 vilivyochukua fomu,
wamekidhi matakwa ya sheria ya mchakato huo, hivyo wanaruhusiwa kuanza
kampeni rasmi kesho.
Amewataja wagombea waliopitishwa na NEC
ni Dk. John Magufuli (CCM), Edward Lowassa (Chadema), Fahmi Dovutwa
(UPDP), Macmillan Lyimo (TLP) na Chief Lutalosa Yemba (ADC).
Wengine ni Anna Mghwira (ACT-Wazalendo) na Hashimu Rungwe (Chaumma) na Malik Kasambala (NRA).
CREDIT: UKURASA WA HABARI
No comments:
Post a Comment