
Mheshimiwa Edward Lowassa akitoa shukrani kwa wana-CCM Tabora waliomdhamini leo hii.
Hali hiyo ilifanya Lowassa kutoamini kile ambacho alikuwa akielezwa na kuishia kujawa na furaha.
Awali msafara wa mapokezi yake yalianzia nje ya mji wa Tabora eneo la kata ya Ipuli ambapo msafara wake ulifika eneo hilo majira ya saa 01:40 na kuungana na msafara uliotoka mjini na zaidi ya gari 100 na msafara huo ulianza safari ya mjini.
Msafara huo ulizunguka maeneo kadhaa ya mjini,soko kuu Isevya na kufikia ofisi za CCM mkoa wa Tabora na ulisimama kwa muda ambapo aliingia ofisi hiyo kusalimu na kuongea na viongozi wa CCM mkoa.
Akihutubia wananchi baada ya kudhaminiwa aliwashukuru umati uliojitokeza kumlaki na kumsikiliza na kutamka mapokezi hayo yamefunika maeneo yote ya mikoa aliyopita kudhaminiwa.
“Jamani siku zote imani huzaa imani…….nami imani hiyo nitaitoa kwenue,” alisema.
Alisema anagombea kwa sasa anachukia umasikini kwani hata umasikini wa mkoa wa Tabora na watu wake anautambua hasa kwenye tumbaku.
Alisema umasikini atauondoa kwa watanzania kuelekea maendeleo kwa njia ya mchakamchaka na atakayeshindwa akaye pembeni.
Lowassa alisema mtu yoyote ama mtendaji ambaye atashindwa kusimama imara kuondoa umasikini kwa njia ya mchakamchaka akae pembeni atupishe.
Hata hivyo Lowassa aliomba wananchi waliokusanyika kwa maelfu kwa maelfu wahakikishe wanajiandikisha kwenye daftari la wapiga kura.
Aidha alisistiza wana Tabora kutumia fursa hiyo kujiandikisha na kwamba yeye anapenda wana Tabora kwani alishatawazwa kuwa chifu wa wanyamwezi.
Bashe aibukia mkutanoni
Katika hatua nyingine kabla Lowassa hajaanza kuhutubia alisema ‘hapa ngojeni kwanza kuna mtu hapa kama hatasema chochote hatalala hivyo nakuomba Bashe uje hapa useme.
Aidha mjumbe wa mkutano mkuu CCM taifa Hussein Bashe alipopewa kipazasauti alisema kura za wanaTabora ziko salama kwa Lowassa.
Bashe alisema licha ya kura hizo kuwa salama lakini imebaki kura moja ya mjomba wake akimaanisha kura ya mbunge wa jimbo la Tabora mjini Ismail Aden Rage na kuamsha shangwe.
No comments:
Post a Comment