Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Friday 26 June 2015

WAERITREA WAANDAMANA KUPINGA UTAWALA WA UDHALIMU

Rais Isaias Afeworki
Mamia ya wakimbizi wa Eritrea wanaoishi nchini Ethiopia wameandamana mbele ya majengo ya muungano wa afrika AU wakiitaka muungano huo kuchukua hatua zaidi kumaliza ukiukaji wa haki za kibinadamu nchini mwao.

null
Wanaitaka muungano wa Afrika kuchukua hatua za kupunguza udhalimu nchini Eritrea
Wakiwa wamebeba mabango ya kumkashifu rais wa nchi hiyo, Isaias Afeworki, waandamanaji hao wamesema ukiukaji mkubwa wa haki zao umeendelea nchini Eritrea huku jamii ya kimataifa ikijikokota kuingilia kati.
null
Ripoti ya UN inasema kuwa nci hiyo inatawaliwa kwa hofu
Ripoti ya hivi karibuni ya Umoja wa Mataifa imesema nchi hiyo inatawaliwa kwa hofu na woga mwingi.
Kiongozi wa uchunguzi wa umoja wa mataifa ameitaka mahakama ya makosa makuu ya kivita ICC kuchunguza tuhuma dhidi ya utawala wa rais Afeworki.
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment