Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Friday, 26 June 2015

WAKAZI IGALULA WADAI HAWANA BARABARA

Ujenzi wa barabara mkoani Tabora

Na Hastin Liumba, Uyui 
WAKAZI wa baadhi ya vitongoji na vijiji vya jimbo la Igalula wilayani Tabora ,Uyui mkoani Tabora wamedai maeneo yao yanakabiliwa na ukosefu wa barabara za uhakika hali ambayo inasababisha kukwama kufikiwa kwa maendeleo.

Wakiongea kwa nyakati tofauti kwenye mkutano wa hadhara mbele ya mwenyekiti wa CCM wilaya ya Uyui Musa Ntimizi walisema wamechoka na hali hiyo.
Wananchi hao ni kutoka vitongoji vya Chaya kata ya Tura, Vitongoji vya Usasi na Kagua kijiji cha Itaga, kata ya Lutende, kitongoji cha Legezamwendo,kitongoji cha Migongwa kata ya kata ya Loya na kijiji cha Genge sita kata ya Kizengi.
Wananchi hao walisema kero wanazo nyingi lakini barabara ni jambo la kuangaliwa kwa ukaribu hasa kipindi cha masika imekuwa kero kuu kwao.
Walisema wanazalisha mazao tena mengine ya kibiashara na kwamba kilio hicho pia wameshawahi kumfikishia katibu mkuu CCM taifa Abdulrahaman Kinana na alihaidi kufikisha kilio chao.
Wananchi hao walisema kipindi cha masika hali huwa mbaya kwani kuna maeneo mengine hakuna madaraja na knamama wajawazito hufariki kwa kukosa huduma za afya huku kukikosekana usafiri wa uhakika.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Uyui Musa Ntimizi kwa upande wake alisema kilio hicho hata yeye mwenyewe kajionea hali mbaya ya barabara za jimbo hilo na lile la Igalula na  na lile la Tabora Kaskazini atafikisha kwa wahusika kwa hatua.
Alisema maeneo mengi aliyopita ya barabara nyingi ni za hatari mno na kwamba ipo haja barabara hizo kuangaliwa upya.
Alisema wananchi hao wanateseka kwa kukosa barabara za uhakika kipindi cha masika hivyo kama wanafikia mahali wanalalamika kiasi hicho wanaweza kutuhukumu CCM kwa kukosa huruma ya kusaidia kuwaletea maendeleo yao.
Mbunge wa jimbo la Igalula Dk Athuman Mfutakamba alipoulizwa alijibu ni kweli hali ya barabara jimboni kwake siyo nzuri lakini amekuwa akipambana kufikisha kilio chao kunakohusiska.

No comments:

Post a Comment