Mshambuliaji wa Brazil Neymar atakosa michuano yote ya kombe la Copa America baada ya kupigwa marufuku ya mechi nne.
Mchezaji huyo wa miaka 23 kutoka klabu ya Barcelona alionyeshwa kadi nyekundu kwa kuzozana na wachezaji wa Colombia baada ya Brazil kushindwa na Colombia 1-0 katika mechi ya makundi.
Alikuwa amepewa marufuku ya mechi moja ambayo ingemlazimu kukosa mechi ya mwisho ya makundi dhidi ya Venezulea siku ya jumapili.
Lakini shirikisho la soka la Marekani ya kusini limekiangazia tena kisa hicho na kuongeza adhabu hiyo.
Neymar alionyeshwa kadi nyekundu baada ya kuupiga mpira kimakusudi kwa lengo la kumgonga mchezaji wa Colombia Pablo Armero baada ya kipenga cha mwisho cha mechi kabla ya kumpiga kichwa mchezaji mwengine ambaye alimsongelea.
Vyombo vya habari vya Brazil vinasema kuwa alimkaripia refa kabla ya kuingia katika chumba cha mapumziko.
CREDIT: BBC
No comments:
Post a Comment