Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Friday, 26 June 2015

WANANCHI UYUI WALIA NA MBUNGE WAO

Dk. Athumani Mfutakamba, Mbunge wa Uyui
Na Hastin Liumba, UyuiWAKAZI wa kata ya Loya wilaya ya Uyui mkoani Tabora wamemlalamikia mbunge wao Dk. Athumani Mfutakamba kwa kutowatembelea tangu walipomchagua.

Malalamiko hayo waliyatoa kwenye mkutano wa hadhara kufuatia ziara ya mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Tabora (Uyui) Musa Ntimizi mkoani hapa.
Wakazi hao walimueeleza mwenyekiti huyo kuwa wengine wlimchagua bila kumjua na wengine walisema walimuona siku moja tu na kwamba kero zao wamwambie nani.
Wananchi hao toka vijiji vya Legezamwendo na Migongwa walisema hawana shule kisi watoto wao kutembea umbali wa kilomita tisa (9) kwenda shule n wengine huishia njiani na kuacha shule.
Aidha walibainisha kuwa hata Barabara yenyewe ni njia ya Ng`ombe haipitiki kwa urahisi hasa kipindi cha masika na huduma za afya nazo shida kwani wanalazimika kutafuta huduma hizo umbali mrefu.
“Mbunge wetu hatumuoni na wengine hatumjui hajatembele huku muda mrefu sasa tumwambie nani kero zetu tunaomba tusaidiwe katika haya.” walisema.
Wakazi hao ambao kwa kitongoji cha Legezamwendo kina wakazi 3,683 na Migongwa wakazi 2,160 walimuomba mwenyekiti huyo kuwasilisha malalamiko hayo serikalini kwani wameshajitolea nguvu kazi kuanza ujenzi wa shule zao hivyo wanaomba kuungwa mkono.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Uyui Musa Ntimizi aliwaomba wananchi hao kuwa watulivu na malalamiko yao atayafikisha kwa mkurugenzi wa halmashauri ya Tabora (Uyui) Hadija Makuwani na mbunge wa jimbo la Igalula Dk Atuman Mfutakamba kwa utatuzi.
Ntimizi alipongeza wananchihao kwa kuanzisha ujenzi wa shule yao hivyo alichangia bati bandari moja yenye thamani ya sh 256,000.
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Tabora (Uyui) Hadija Makuwani alipoulzwa alisema hana taarifa hivyo aliahaidi kufuatilia suala hilo kupata majibu yake na kuchukua hatua.
Mbunge wa jimbo la Igalula Dk Athuman Mfutakamba alipotafutwa kujibu malalamiko ya wapiga kura wake alisema wananchi waache uzushi na wanatumwa sana.
Aalisema wanaosema hawajui mbunge wao wengi wao wanakuwa kwenye misitu wakirina asali hivyo hao hawaweze kumjua mbunge wao.
Alisema amechimba visima,umeme, kupeleka godoro baadhi ya zahanati,maji na amekuwa akitumia fedha zake na za mfuko wa jimbo.
Aidha alongeza baadhi hasa Legezamwendo wamekasirika kwa kuwa wamekosa kijiji hivyo hao ni wazushi tu wanatumwa na jimbo la Igalula lina vijiji 94 ambavyo amvisaidia sana.
Alisema yeye amefanya makubwa jimboni kwake na anakwenda hatua kwa hatua na anasubiria bajeti ya mfuko wa jimbo fedha zikitoka ataendelea kuchimba visima na kuboresha hudum za elimu na barabara.

No comments:

Post a Comment