Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday 30 June 2015

U15 YAREJEA DAR KUTOKA MBEYA

Peter Manyika, kocha wa U15


Kikosi cha timu ya Taifa cha vijana wenye umri chini ya miaka 15 (U-15) leo kinarejea jijini Dar es salaam kikitokea mkoani Mbeya ambapo jana kiliibuk ana ushindi wa ushindi wa mabao 4-1.U15 ambayo inaandaliwa kwa ajili ya kuwania kufuzu kwa fainali za vijana chini ya miaka 17 barani Afrika kilikua na ziara ya michezo ya kirafiki miwili jijini Mbeya ambapo katika mchezo wa awali pia kiliibuka na ushindi wa mabao 3-0.

Mara baada ya kurejea leo jioni jijini Dar es salaam, kambi ya timu hiyo itavunjwa mpaka watakapokutana tena mwisho wa mwezi ujao kwa ajili ya kuelekea visiwani zanzibar kwa jili ya michezo ya kirafiki.

Lengo la michezo hiyo ya kirafiki ni kutoa nafasi ya kocha Bakari Shime kutambua uwezo wa vijana wake na kuongeza wachezaji wengine katika kikosi hicho kisha kuandaa kikosi bora kitakachoshirki kuwania kufuzu kwa fainali hizo zitakazofanyika nchini Madagascar mwaka 2017.


PRESS CONFERENCE
Baraza la Vyama vya Soka kwa Nchi za Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) kesho siku ya jumatano kupitia kwa viongozi wake wa ngazi za  juu, wataongea na waandishi wa habari saa 5 kamili asubuhi katika ukumbi wa mikutano wa TFF uliopo Karume.

Waandishi wote wa habari mnaombwa kuhudhuria mkutano huo bila kukosa.


IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

No comments:

Post a Comment