Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday 23 June 2015

NTIMIZI AMWAGA VIFAA VYA MICHEZO VYA MILIONI 40

Mussa Ntimizi
Na Hastin Liumba, Uyui
MWENYEKITI wa chama cha mpira wilaya ya Uyui mkoani Tabora Musa Ntimizi amemwaga vifaa vya michezo katika wilaya ya Uyui vyenye thamani ya Shs. milioni 40.


Vifaa alivyotoa kwenye timu za mpira wa miguu wilayani humo ni jezi seti 50 na mipira 200 vyote vikiwa na thamani y ash milioni 40.
Ntimizi ambaye ni mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tabora (Uyui) alitoa vifaa hivyo kama mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu wilaya hiyo ikiwa ni sehemu kama mdau wa michezo na ahadi aliyotoa, na kukuza vipaji vilivyoko wilayani kwake.
Akiongea kwenye ziara yake wilayani Uyui Ntimizi alisema ataendelea kutoa vifaa vya michezo kwa timu za wilaya hiyo kwani kuna vipaji lukuki vinavyopaswa kuendelezwa.
“Mimi licha ya kuwa mwenyekiti wa chama cha soka wilayani kwangu bado ni mdau mkubwa wa soka hivyo naguswa mno kuona vijana wanakosa fursa ya michezo …..ni lazima nisaidie eneo hili.” alisema Ntimizi.
Akielezea zaidi wakati akiongea kwenye maeneo aliyopita kwenye ziara hiyo aliwataka vijana kujitoa kushiriki michezo hasa mpira wa miguu.
Alisema michezo ni ajira,afya,furaha na hukutanisha wadau kwa pamoja kama ndugu hivyo yeye atakuwa pamoja nao.
Alisema yeye kama mwenyekiti chama Uyui bado ni mlezi wa timu zote zilizoko kwenye wilaya yake hivyo atahakikisha vijana hao ama timu zinaendelezwa na kufikia hatua ya kutoa timu wilayani kwake kwenda ligi kuu ya Vodacom Tanzania.
Aliwaomba wadau wa soka akiwemo wawilaya hiyo kumuunga mkono ili vipaji vilivyoko jimbo la wilaya ya Uyui vinakuzwa.
Kwa upande wao wawakilishi wa timu kwa nyakati tofauti walishukuru hekima za mwenyekiti wa chama soka wilaya kwa hatua hiyo.
Walisema toka historia ya wilaya hiyo kuanzishwa hawakuwahi kupatiwa msaada wa vifaa vyenye thamani kubwa kama hiyo.

No comments:

Post a Comment