Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Monday 22 June 2015

GOOGLE YAKUBALI KUONDOA PICHA ZA UCHI


Waathiriwa wa picha za ngono katika mtandao wa Google wataruhusiwa kutuma ombi kwa kampuni hiyo la kuziondoa picha hizo.

Picha hizo zitaendelea kuwa katika mtandao huo lakini hazitaorodheshwa katika picha wakati wateja watakapozitafuta.
Makamu wa rais wa kampuni hiyo Amit Singhal amesema kuwa mpango huo utashirikisha picha za uchi na zile zenye uchafu mkubwa.
Google hapo awali ilikataa jaribio la kuitaka kuondoa picha kama hizo katika picha zilizoorodheshwa katika mashine yake ya utafutaji.
Mpango huo mpya unatarajiwa kuanza kufanya kazi katika kipindi cha wiki chache zijazo.
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment