Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday 23 June 2015

WATU 20 WAFARIKI DUNIA KATIKA SHAMBULIO NIGERIA

Shambuliao jijini Maiduguri
Watu ishirini wamefariki dunia kutokana na shambulio la kujitoa muhanga katika soko la wachuuzi wa samaki lililokuwa limefurika watu eneo la Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.

Watu wengi walikuwa wameumia vibaya wakati mwanamke mmoja alipojiripua kati kati ya watu katikati mwa mji wa Maiduguri.
Mashuhuda wa ajali hiyo wameeleza kwamba mwanamke mwingine alijaribu kushambulia eneo hilo hilo kwa jaribio la kujilipua lililoshindwa, lakini baadaye aliamua kukimbilia msikitini, ambapo alikufa baadaye baada ya mabomu aliyojifungia kuripuka.
Mpaka sasa haijajulikana kwamba ni nani anayeendesha mashambulio hayo kati ya makundi ya kigaidi yakiwemo Boko Haram ambalo lina nguvu kubwa Kaskazini Mashariki mwa Nigeria, ambapo mara kadha wamekuwa wakitumia watu wanaojitoa muhanga na vilipuzi.
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment