Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Sunday 28 June 2015

BLATTER ASEMA, HAKUJIUZULU KAMA RAIS WA FIFA!

Sepp Blatter
Rais wa shirikisho la soka duniani Sepp Blatter amekariri kuwa hakujiuzulu kama rais wa shirikisho hilo.

Kiongozi huyo Mswissi mwenye mri wa miaka 79 alikuwa amedhaniwa kujiondoa madarakani juni tarehe 2 kufuatia kashfa kubwa ya ufisadi ulajirushwa na matumizi mabaya ya madaraka iliyokumba shirikisho lake lakini sasa anaonesha dalili za kubadili mtazamo huo.
Blatter ambaye ameiongoza FIFA kwa miaka 17 alikuwa ametangaza kuwa atajiondoa mbele ya kamati kuu ili kufanyike uchunguzi wa kina katika FIFA lakini sasa amelikumbusha jarida moja la Uswisi BLICK kuwa yeye ndiye rais wa FIFA na kuwa aliweka hatima yake mikononi mwa kamati kuu ya shirikisho katika mkutano wa dharura.
null
Hakuna mipango ya Blatter kuelekea Canada kwa Fainali ya kombe la Dunia la wanawake
Blatter anadhaniwa kuwa anafikiria kuwania tena uongozi wa shirikisho hilo.
Tuhuma za udhabirifu wa fedha ufisadi na ulaji rushwa ulianza katika ileile wiki ambayo Blatter alichaguliwa ikiendeshwa na Marekani.
Lakini punde baada ya uchaguzi utawala nchini Uswisi nao ukaanzisha uchunguzi sambamba wa ulaji rushwa na ufisadi dhidi ya maafisa wakuu katika shirikisho la soka duniani FIFA.
Blatter alitangaza kuwa anajiondoa uongozini ili kuruhusu uchunguzi ufanyike siku nne tu baada ya kuchaguliwa upya kwa hatamu ya uongozi wa FIFA.
null
Ng'o Siondoki !
Kufuatia uchunguzi unaoendelea hakuna mipango na dalili zozote kuwa Blatter ama katibu mkuu wa FIFA
Jerome Valcke atakuwa mjini Ontario, Canada katika fainali ya kombe la dunia kwa wanawake.
Kwa kawaida Blatter angekuwa huko ilikutoa zawadi ya kombe la dunia kwa timu itakayoibuka mshindi lakini hadi kufikia sasa hakuna mipango yoyote ya ziara hiyo.
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment