Mbayuwayu Koo-jeupe (White-throated Swallow)
Na Daniel Mbega
RAIS wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, alipata kusema wakati mmoja
kwamba, “Akili za Mbayuwayu, changanya na zako!” Wagogo wanamwita 'Samamba', sijui wewe kwa lugha ya kabila lako wanaitwaje!
Kauli hii ina maana kubwa
sana, kwani wengi tunaamini kwamba ndege aina ya Mbayuwayu wana akili sana kwa
jinsi wanavyoruka angani kwa kasi ya ajabu kukamata wadudu.
Wakati mwingine unaweza
kudhani ndege huyo anakufuata, lakini anakuja kasi na anapokukaribia anakula
kona kali.
Enzi zile nikiwa mdogo
nakumbuka tulikuwa tunapata taabu sana kuwapiga kwa sababu ni ndege wajanja.
Tulikuwa tunashika fimbo ndefu na kuwavizia, lakini wapi, kuwapata ni shida.
Naam. Hao ndio Mbayuwayu
au kwa jina linguine wanaitwa Vijumbamshale. Ndege hawa wanatoka katika Himaya
ya Animalia (Wanyama), Faila ya Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva
mgongoni), Nusufaila ya Vertebrata
(Wanyama wenye uti wa mgongo), Ngeli ya Aves
(Ndege), Oda ya Passeriformes (Ndege
kama Shomoro), Familia ya Hirundinidae
(Ndege walio na mnasaba na Mbayuwayu).
Spishi nyingine zinaitwa Kinega
au Kizelele. Wanafanana na Teleka lakini hawa wako katika oda yao yenyewe, Apodiformes.
Zipo Jenasi nyingi za
ndege hawa ambazo ni Atticora Boie, 1844;
Cecropis; Cheramoeca Cabanis, 1850; Delichon Horsfield & Moore, 1854;
Haplochelidon Todd, 1929; Hirundo Linnaeus, 1758; Neochelidon P.L. Sclater,
1862; Notiochelidon S.F. Baird, 1865; Petrochelidon Cabanis, 1850; Phedina
Bonaparte, 1855; Progne Boie, 1826; Psalidoprocne Cabanis, 1850; Pseudhirundo
Sundevall, 1850; Pseudochelidon Hartlaub, 1861; Ptyonoprogne Reichenbach, 1850;
Riparia T. Forster, 1817; Stelgidopteryx S.F. Baird, 1858; na Tachycineta Cabanis, 1850.
Mbayuwayu wana miguu
mifupi kama Teleka lakini mabawa yao ni mafupi zaidi na spishi nyingi zina
rangi kama nyekundu, buluu na/au zambarau. Hutua mara kwa mara. Hukamata wadudu
wakiruka angani.
Spishi kadhaa hutaga
mayai yao ndani ya mashimo asilia au matundu yaliyoachwa na vigong'ota. Spishi
nyingi nyingine huchimba tundu lao katika maada isiyo gumu kama vile ukingo wa
mto. Spishi za jenasi za Hirundo,
Ptyonoprogne, Cecropis, Petrochelidon na Delichon hujenga matundu yao ya matope kupambana na ukuta wa jabali
au jengo kwa kawaida karibu na sehemu inayochomoza kama paa la jengo. Jike
hutaga mayai kati ya 2-5.
Spishi za Mbayuwayu zinazopatikana barani Afrika ni:
Mbayuwayu Michirizi Mdogo
(Lesser Striped Swallow)
Mbayuwayu Michirizi
Mkubwa (Greater Striped Swallow)
Mbayuwayu Kiuno-chekundu
(Red-rumped Swallow)
Mbayuwayu Tumbo-jekundu (Rufous-chested
Swallow)
Mbayuwayu Mkubwa (Mosque
Swallow)
Mbayuwayu-kaya (House
Martin)
Mbayuwayu Habeshi
(Ethiopian Swallow)
Mbayuwayu wa Angola
(Angolan Swallow)
Kizelele-milima (Montane
Blue Swallow)
Mbayuwayu Rangi-mbili
(Pearl-breasted Swallow)
Mbayuwayu Mbawa-mabaka
(Pied-winged Swallow)
Mbayuwayu Kidari-chekundu
(Red-chested Swallow)
Mbayuwayu Mkia-mweupe
(White-tailed Swallow)
Kizelele Koo-jeupe
(White-throated Blue Swallow)
Mbayuwayu Mweusi-mwekundu
(Black-and-rufous Swallow)
Mbayuwayu wa Ulaya (Barn
Swallow)
Mbayuwayu Mkia-sindano
(Wire-tailed Swallow)
Mbayuwayu-misitu (Forest
Swallow)
Mbayuwayu wa Bahari ya
Shamu (Red Sea Cliff Swallow)
Mbayuwayu wa Preuss
(Preuss's Cliff Swallow)
Mbayuwayu Koo-jekundu
(Red-throated Cliff Swallow)
Mbayuwayu Kusi (South
African Cliff Swallow)
Mbayuwayu-visiwa
(Mascarene Martin)

Mbayuwayu wa Brazza
(Brazza's Martin)
Mbayuwayu Kichwa-cheupe
(White-headed Saw-wing)
Mbayuwayu-milima
(Mountain Saw-wing)
Mbayuwayu Mkia-mraba
(Square-tailed Saw-wing)
Mbayuwayu wa Fanti (Fanti
Saw-wing)

Mbayuwayu Mashariki
(Eastern Saw-wing)
Mbayuwayu Mweusi (Black
Saw-wing)

Mbayuwayu Kiuno-kijivu
(Grey-rumped Swallow)
Mbayuwayu-mtoni (African
River Martin)
Mbayuwayu-mawe (Rock
Martin)
Mbayuwayu-mawe wa Ulaya
(Eurasian Crag Martin)
Kinega Miraba (Banded
Martin)
Kinega wa Kongo (Congo
Sand Martin)
Kinega Koo-kahawia (Plain
Martin)
)
Kinega-mchanga (Common
Sand Martin)
Spishi za mabara mengine
* Alopochelidon fucata
(Tawny-headed Swallow)
* Atticora fasciata
(White-banded Swallow)
* Atticora melanoleuca
(Black-collared Swallow)
* Cecropis badia
(Rufous-bellied Swallow)
* Cecropis striolata
(Striated Swallow)
* Cheramoeca leucosternus
(White-backed Swallow)
* Delichon dasypus (Asian
House Martin)
* Delichon nipalense
(Nepal House Martin)
* Hirundo neoxena
(Welcome Swallow)
* Hirundo tahitica
(Pacific Swallow)
* Neochelidon andecola
(Andean Swallow)
* Neochelidon tibialis (White-thighed
Swallow)
* Notiochelidon
cyanoleuca (Blue-and-white Swallow)
* Notiochelidon flavipes
(Pale-footed Swallow)
* Notiochelidon murina
(Brown-bellied Swallow)
* Notiochelidon pileata
(Black-capped Swallow)
* Petrochelidon ariel
(Fairy Martin)
* Petrochelidon fluvicola
(Streak-throated Swallow)
* Petrochelidon fulva
(Cave Swallow)
* Petrochelidon nigricans
(Tree Martin)
* Petrochelidon
pyrrhonota (Cliff Swallow)
* Petrochelidon
rufocollaris (Chestnut-collared Swallow)
* Progne chalybea (Grey-breasted
Martin)
* Progne cryptoleuca
(Cuban Martin)
* Progne dominicensis
(Caribbean Martin)
* Progne elegans
(Southern Martin)
* Progne modesta
(Galapagos Martin)
* Progne murphyi
(Peruvian Martin)
* Progne sinaloae
(Sinaloa Martin)
* Progne subis (Purple
Martin)
* Progne tapera
(Brown-chested Martin)
* Pseudochelidon
sirintarae (White-eyed River Martin)
* Ptyonoprogne concolor
(Dusky Crag Martin)
* Riparia diluta (Pale
Martin)
* Stelgidopteryx
ruficollis (Southern Rough-winged Swallow)
* Stelgidopteryx
serripennis (Northern Rough-winged Swallow)
* Tachycineta albilinea
(Mangrove Swallow)
* Tachycineta albiventer
(White-winged Swallow)
* Tachycineta bicolor
(Tree Swallow)
* Tachycineta
cyaneoviridis (Bahama Swallow)
* Tachycineta euchrysea
(Golden Swallow)
* Tachycineta leucorrhoa
(White-rumped Swallow)
* Tachycineta meyeni
(Chilean Swallow)
* Tachycineta stolzmanni
(Tumbes Swallow)
* Tachycineta thalassina
(Violet-green Swallow)
Kama unawajua ndege hawa kwa majina ya asili (kilugha)
tafadhali usisite kuniandikia kupitia barua-pepe: brotherdanny5@gmail.com au
simu/whatsapp/telegram 0656-331974
No comments:
Post a Comment