Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday, 4 June 2015

CHUO CHA MUSOMA UTALII SASA KUSOMESHA YATIMA

Displaying IMG_20150420_161448.jpg
Mkurugenzi wa chuo cha Musoma utalii Shaban Mrutu
 Displaying IMG_20150420_171126.jpg
Sehemu ya mbele ya jengo la Chuo cha Musoma Utalii. (Picha zote na Hastin Liumba)


Na Hastin Liumba, Tabora
UMASIKINI ni kitu ambacho siku zote kimekuwa kikikwamisha mambo mengi miongoni mwa jamii nchini.

Hali hiyo imekuwa ni kikwazo cha kufikiwa kwa malengo yanayokusidiwa katika mikakati ya maendeleo tarajiwa. Lakini maendeleo hayawezi kuja kirahisi bila ya jamii kupata elimu bora.
Wengi wa wazazi na walezi wameshindwa kusomesha watoto kutokana na kukosa uwezo wa kusomesha na hali hiyo imesababisha kaya nyingi kuwa masikini.
Mkurugenzi wa chuo cha Musoma Utalii mkoani Tabora Shaban Mrutu alisema hayo wakati akifanya mahojiano na mwandishi wa makala hii.
Mrutu alisema kwa kutambua umuhimu wa elimu katika jamii alianzisha mpango wa kusomesha  watoto yatima, watoto waishio kwenye mazingira magumu na wasiojiweza.
Alisema chuo kimekuwa na mfuko maalumu wa kusomesha watoto hao kwa mpangilio ulio bora ambao utashirikisha serikali na wadau wa elimu, mpango huu ulianza mwezi Januari 2014.
Alibainisha watoto hao wanachukuliwa wakiwa na sifa maalumu za kujiunga na vyuo na watachukuliwa watoto wanne kila muhula.
Alibainiaha masomo watakayochukua ni yale ambayo yanayofundishwa chuoni hapo na kozi hizo zitaendana na sifa ya mtoto atayechukuliwa.

Kozi zitolewazo chuoni
Aidha mkurugenzi huyo alitaja chuo kinatoa kozi wanazotoa kuwa ni Tour Guide and Administration, Tourism and Airline Management, Travel Studies and Tour Operation.
Alitaja nyingine ni International Hotel Managemet, Food and Beverage Services and Sales, Food Production Cooker and Bakery, Front Office Operation, Information and Communication Technology (ICT).
Mrutu anaongeza kozi nyingine ni Nurcsery School Teacher (Early Childhood Education), Journalism Radio and TV Broadcasting),Secretarial Course, Records Management, Procurement and Supply Management na
Business Administration na kozi hizi ni kwanga ngazi ya Cheti (NTA Level 4).
Aidha aliongeza zipo kozi fupi za Computer in office Application, Computer Maintenance and Electronics, Computer Knowledge na Graphic and Disegn.
Nyingine ni Music Prodactions, Elementary/foundation Course, Entrepreneurship Development na English, French and Italian.
Mrutu alibainisha kuwa chuo pia kinatoa kozi ngazi ya Diploma (NTA) Level 5 &6 Tour Guiding and Administration,Imformation Communication Technology,Early Childhood care and Education, Journalism, Radio& TV Broadcasting, Hotel Management, Business Administration, Records Management, Full Secretarial Course na Diploma in Primary School Education.
Mrutu alibainisha mpango huo wa kusomesha watoto wasiojiweza unahusisha mwanafunzi anayekubali kuishi bweni ama kutwa na atalipiwa gharama zote.

Vigezo vitakavyotumika
Mrutu anasema mtoto atapatikana kwa kupitia vigezo vitakavyowekwa ambavyo ni barua za utambulisho toka kwa mwenyekiti wa mtaa,kitongoji,kijiji na mkuu wa wilaya.
Alisema hadi sasa chuo kimeshachukua watoto wanne ambao wanaendelea na masomo hadi sasa na maendeleo yao ni mazuri.
“Nimeamua kusomesha watoto hawa kwa kutambua umuhimu wa elimu hasa katika kipindi hiki cha mabadiliko makubwa ya Sayansi na Teknolojia duniani.”aliongeza.
Alisema hatua hiyo ina lengo la kusaidia watoto wenye nia na dhamira ya kusoma lakini hawana uwezo wa kupata fursa hiyo hasa kutokana na wazazi na walezi kuwa na hali duni.

Changamoto anazokumbana nazo
Mrutu anasema licha ya mpango kuwenda vyema bado amekuwa akikumbana na changamoto kadhaa ambazo ni baadhi ya vijana wanaokuja wanakosa sifa na vigezo.
Alitaja nyingine ni idadi ya vijana wanaokuja inakuwa kubwa kuliko uwezo wa mfuko wa kusomesha watoto hao huku wengine wakigushi barua toka kwa wenyeviti wa mitaa,vitongoji na vijiji.
Licha ya hayo amekuwa akifatilia kwa ukaribu ili watoto waliolengwa wanachukuliwa na siyo kuchukua watoto wasiokuwa kwenye mpango.
Aidha alishauri viongozi ngazi za mtaa,vitongoji na vijiji wasitumike vibaya kubaini watoto wanaowapa barua za kutambulisha kama familia haina uwezo.

Malengo ya mpango huo
Mrutu anasema malengo ya mpango huo alioanzisha ni kutafuta wafadhili ili kuweza kuchukua idadi ya watoto wengi wenye uhitaji.
Alisema anakusudia kuboreha mfuko huo ili kuweza kuchukua watoto 10 kila muhula lakini kabainisha anahitaji kuungwa mkono na wadau,serikali na wafadhili kufanikisha hilo.
Alisema uwepo wa chuo hiki kanda ya magharibi kutasaidia watumishi sekta ya utalii katika maeneo mbalimbali kanda hii kuendelea kupata elimu bora na kuboresha huduma kwa wananchi.
Mrutu anasema mpango huo wa chuo ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya serikali ya CCM pamoja na mambo mengine inatilia mkazo upatikanaji wa elimu bora mkoani Tabora na kwa watanzania wote.
Alibainisha malengo mengine ni watoto watakaofanya vyema na kufaulu vizuri masomo yao watasaidiwa kutafutiwa ajira.
Alisema ufaulu wa wanafunzi siyo suala la mwalimu na mwanafunzi pekee bali ni wajibu wa jami nzima.
Mkurugenzi huyo anasema jamii inakuwa na wajibu wa kusaidia maeneo mbalimbali hususani upatikanaji wa mazingira bora ya kujifunzia na kufundishia.
Alibainisha mpango huo umelenga pia utekelezaji wa mpango wa matokeo makubwa sasa (BRN) pamoja na kutathimini utekelezaji wa mkakati.

Wito kwa jamii
Mkurugenzi huyo anatoa wito kwa jamii, wafadhili, wadau wa elimu na serikali kusapoti mpango wake ili kunusuru watoto ambao wana nia ya kusoma lakini wanakosa haki hiyo kwa kutokuwa na uwezo wa kifedha.
“Kundi hili la watoto wasiojiweza ni kubwa nchini hivyo ninahitaji kujipanga zaidi na hili linawezekana hata kwa taasisi nyingine kama yangu tujitoe tu.” aliongeza.
Alisema anaiomba serikali kuunga mkono hatua hiyo kwani itasaidiwa vijana ambao wana sifa na uhitaji wa elimu kushindwa kufikia malengo yao.

hastinliumba@gmail.com-0788390788

No comments:

Post a Comment