Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday, 4 June 2015

UJUMBE WA LEO: HII KAZI INA LAANA!!!

Ndugu zangu,
Kazi ndiyo msingi wa maisha. Kuna kazi halali na haramu. Halali ni ile ambayo hata jamii inakubali kwamba inastahili kufanywa. Mungu pia ameibariki! Hata unapoifanya moyo wako unakuwa na amani na unapopata ujira wake kamwe huwezi kuifuja mali hiyo.
Kazi za aina hii zaweza kuwa kuzoa mchanga, kuzibua mifereji, kupiga debe kwenye vituo vya mabasi, ajira za kawaida ofisini, mashambani na migodini, lakini hata kilimo, ufugaji na kuuza mkaa.
Lakini kazi haramu, ama yenye laana, ni ile ambayo iko kinyume na maadili ya jamii. Ujambazi, wizi, ukahaba, ufisadi na rushwa ukiwa katika kazi rasmi na kadhalika, ni kazi ambazo siyo halali hata kama zina kipato.
Wengi wanaofanya kazi za aina hii, hata kama watafanikiwa na kuwa na maendeleo katika jamii, lakini taswira yao huwa mbaya kwa jamii husika. Watu wanakuepa, hasa wakijua unafanya kazi gani.
Wanaofanya kazi hizi hata ujira wao huutapanya ovyo licha ya kwamba wameupata katika mazingira magumu. Mioyoni mwao wanasema, watapiga dili tena na kupata fedha ama mali nyingine.
Lakini mwisho wa siku, maisha yao huisha kiharamu hivyo hivyo.Naamini sote tunafahamu jinsi kibaka anavyoteketezwa kwa moto angali hai na mambo kadha wa kadha.
Ndugu zangu,
Ni wajibu wetu kutafakari kazi tunazozifanya kama zina baraka ama laana!
Huu ni ujumbe wangu wa leo.

Ndugu yenu,
Daniel Mbega,
Igunga
04/06/2015

No comments:

Post a Comment