Mmoja wa kijana ambaye alifika kushuhudia tukio hilo akipanda juu ya Ghorofa baada ya kunusurika kudondokea katika moto huo
Mbele ni Gari la zima moto likiwa limefanya juhudi za kuzima moto , hapa wakiondoka kufuata maji mengine ili kuendelea na zoezi la kuzima moto huo
Moto ukiendelea kuwaka katika Bohari hilo
Baadhi ya Mashuhuda wakishuhudia tukio hilo la kuwaka kwa Bohari
Magari yakiwa yameruhusiwa kuendelea na safari baada ya moto huo na moshi mkubwa kupungua
Picha na Fredy Njeje/Blogs za mikoaBohari moja ambalo lilikuwa la kuhifadhia mataili pamoja na vifaa vyenginevyo vya magari lililopo Sinza Lego ambalo mmiriki wake hakufahamika kwa mara moja limeteketea kwa moto ambapo kwa mujibu ya wenyeji wa eneo hilo wamedai kuwa chanzo cha moto huo ni mataili. Pia katika eneo hilo kuna Gereji ambayo haikuathirika na moto huo mkubwa, mpaka jioni hii kikosi cha kuzima moto kilikuwa eneo la tukio kuendelea kusaidiana na wananchi kuhakikisha moto huo unazimika. Taarifa kamili itatolewa na Jeshi la Polisi.
No comments:
Post a Comment