Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday, 9 June 2015

"WAANDISHI WA HABARI TUMIENI TAALUMA YENU"

Mussa Ntimizi

Na Hastin Liumba,TaboraMWENYEKITI wa CCM wilaya ya Uyui Mkoani Tabora Mussa Ntimizi amewataka waandishi wa habari kufanya kazi kwa kutumia weredi na taaluma yao  na siyo kutumika kisiasa kwa maslahi ya mtu au watu Fulani.


Hayo amebainisha hayo wakati akizungumza na vyombo vya habari ofisini kwake alipokuwa akitoa taarifa kuhusu hali ya kisiasa katika wilaya hiyo.
Alisema kuwa hali ya kisiasa katika wilaya yake iko vizuri kwani amefanya kazi kubwa ya kuhakikisha katika chaguzi za serikali za mtaa,amekuwa wa kwanza kimkoa na anaamini katika uchaguzi mkuu atafanya vizuri zaidi.
Alisema endapo waandishi wa habari watakubali kutumika wanaweza kuleta maafa makubwa ndani ya jamii kwani jamii nzima hutegemea kupata taarifa kutoka kwao hivyo kufanya hivyo watakuwa wanapotosha umma unaowategemea.
“Naamini ninyi ni kioo cha jamii,waalimishaji na wapasha habari kwa jamii ama umma na wananchi wanawakubari kile mnacho kiandika ama kutangaza kuwa ni sahihi hivyo mkikubali kununuliwa na wanasiasa watasababisha kuvuruga amani ya nchi yete.”Alisema Ntimizi.
“Ndugu zangu kumbukeni kuwa mti wenye matunda haukosi kupigwa mawe hivyo mkiona hivyo hamtakiwa kushabikia mnacho takiwa kufanya na kutafuta ukweli wa jambo ili kuondoa msuguano ambayo inaweza kujitokeza”.Alisema Ntimizi.
Katika upande mwingine alisema wilaya yake anakabiliwa na janga la njaa kufutia kuchelewa kuuza zao la tambuku na vijiji tengemea katika kuzalisha mazao ya chakula kutofanikiwa kwa kiwango kinacholidhisha.
Alisema wananchi katika wilaya hiyo hutegemea zao la tambuku kwa aslimia mia lakini kumekuwepo sintofahamu ya soko ya zao hilo na kubakia katika maghala bila kuuzwa hali inayoweza kuathiri maisha ya kazi hao.
Alisema kufuatia hali hiyo ya janga la njaa linalionyemea wilaya hiyo tayari wameandika barua kwa waziri Mkuu kupitia kitengo cha maafa ili waweza kupatia msaada wa chakula ili kunusuru maisha ya wananchi hao ambao ni tegemeo la kesho.

No comments:

Post a Comment