Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday, 9 June 2015

SERIKALI KUBORESHA MIUNDOMBINU YA WASIOONA


Na Hastin Liumba, TaboraSERIKALI mkoani Tabora imesema itaendelea kuboresha miundombinu ya wasioona vijana na watu wazima wasiojua kusoma, kuandika na kuhesabu.

Hayo yalibainishwa na afisa elimu mkoa wa Tabora Juma Mhina wakati akifunga mafuzo ya siku tatu yaliyoshirikisha mikoa ya Tabora, Rukwa,Singida,Manyara na Mwanza.
Mhina alisema mipango ya kuwasaida wasioona itaanzishwa sasa sanjari na kutenga majengo yatakayotumiwa kwa ajili ya masomo yao.
Alisema na kukiri kwa sasa hakukuwa mipango ya kutenga maeneo na majengo yatakayotumika na wasioona kwa ajili ya mafunzo ya.
Aidha alihaidi changamoto zilizopo zitafanyiwa kazi ili kutenga mazingira rafiki kwa wasioona.
Aidha aliwaomba washiriki hao kwenda kuyatumia mafunzo hayo waliyopata kufundisha wengine kwenye vituo watakavyopangiwa.
Awali mratibu wa mafunzo hayo Ibrahim Suleiman alisema wasioona ambao hawajui kuandika,kusoma na kuhesabu wanakabiliwa na changamoto mbalimbali.
Suleiman alitaja changamoto hizo kuwa ni baadhi ya wasioona kufichwa ndani bila kupelekwa shule,kukosekana kwa shule maeneo waishio, kuatisha masomo na kutofahamu uwezekano wa asiyeona kusoma.
Alisema semina hii elekezi imelenga kuwajengea uwezo wa kufahamu mwongozo na wautumie kwa ufanisi na kuimarisha mbinu   na stadi za ufundishaji na ujifunzaji.
Suleiman aliongez kingine ni kutumia vitabu vya kiada na ziada kwa ufanisi, kubuni mbinu za kuwahasisha wanakisomo wapende kujfunza na kuimarisha mfumo wa mawasiliano kati ya mwezeshaji,mkuu wa kituo, jamii na serikali.

No comments:

Post a Comment