Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday, 11 June 2015

TAARIFA YA TUMAINI MSOWOYA KUJIUZURU UENYEKITI WA UVCCM MKOA WA IRINGA

Bi Tumaini Msowoya
TANGU juzi kumekuwa na taarifa za kujiuzuru kwangu nafasi ya Uenyekiti wa Vijana wa CCM (UVCCM)Mkoa wa Iringa baada kikao cha Halmashauri kuu ya CCM Taifa (NEC) chini ya Mwenyekiti wa CCM Taifa,  Rais Dk Jakaya Mrisho Kikwete kuridhia hatua yangu ya kujiuzuru nafasi hii.

Binafsi natoa shukrani zangu za kipekee kwa Mwenyekiti wa CCM Taifa kuridhia uamuzi wangu huo, ambao niliufanya kuondoa mgongano wa kimaslahi unaotokana namimi kuwa mjumbe wa vikao vya uchujaji na uteuzi vya CCM mkoa wa Iringa, huku mume wangu, Ndugu Frank John Kibiki akiwa na nia ya kuwania kuteuliwa na CCM kugombea ubunge katika jimbo la Iringa mjini.
Hii nilizingatia kwamba, kuwamo kwenye vikao hivyo nisingeweza kutenda haki kwa wagombea wengine na hivyo kutotimiza wajibu wangu kikanuni na kikatiba katika kusimamia haki za wagombea wote.
Narudia tena kumshukuru Mwenyekiti wa CCM taifa kuridhia hatua yangu hiyo, kama ilivyokuwa kwa viongozi wengine akiwemo Ndugu, Mwigulu Nchemba aliyejiuzuru nafasi yake ya Unaibu Katibu Mkuu CCM Bara ili kuwe na haki sawa, katika harakati zake za kuomba kuteuliwa kuwania nafasi ya Urais.
Naamini wakati huu nitapata nafasi na uhuru mkubwa wa kushiriki harakati za kupata viongozi wazuri kutoka kwenye chama changu CCM kwa kutimiza wajibu wangu huo wa kikatiba kama mwanachama wa kawaida.
Kwamuda wangu wa uongozi, nimejifunza vitu vingi na kuongezewa ujasiri ikizingatiwa ni mtoto wa kike ambaye nimeitumikia vyema nafasi yangu.
Ninachukua nafasi hii kuwashukuru vijana wote wa CCM mkoa wa Iringa, wanachama wote wa CCM na Viongozi wote kuanzia ngazi ya shina hadi mkoa kwa ushirikiano na upendo wa dhati kwangu kipindi nikiwa madarakani.
Nasisitiza kuwa kujiuzuru kwangu ni kuondoa mgongano wa kimaslahi kikatiba na kikanuni na si vinginevyo.
Umoja ni Ushindi, pamoja tutashinda.
Asante sana
Kidumu chama cha Mapinduzi
TUMAINI MSOWOYA KIBIKI
10/06/2015

No comments:

Post a Comment