Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Saturday, 6 June 2015

MWALIMU KUMRITHI NKUMBA UBUNGE SIKONGE

Mbunge wa sasa wa Sikonge, Said Nkumba


Na Hastin Liumba, SikongeMWALIMU wa shule ya sekondari Mlimani ambaye pia ni mhitimu wa Shahada ya Ualimu kutoka Chuo Kikuu cha Mt. Augustino cha jijini Mwanza, Godfrey Nzalalila amedhamiria kujitosa katika kinyang’anyiro cha ubunge wa jimbo la Sikonge mkoani Tabora kupitia CHADEMA.
Akizungumza katika kikao cha viongozi wa CHADEMA kilichofanyika wilayani humo Nzalalila alisema ameamua kutia nia hiyo ya kumrithi Said Nkumba baada ya kuona mbunge huyo ameshindwa kuleta mageuzi ya kweli ya kimaendeleo katika wilaya hiyo.
Alisema anataka kusimamia na kuhakikisha wafugaji wote wilayani humo wanatengewa mazingira mazuri ili mifugo yao izidi kustawi na kuleta tija kwa maendeleo yao kiuchumi na kijamii sambamba na kuboresha vyanzo vya maji na miundo mbinu yake ili kuwa na maji ya uhakika kwa wakazi wa wilaya hiyo.
Aidha Nzalalila ambaye ni Mjumbe wa Shirika la United Nations Association in Tanzania kituo cha Mwanza, Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Youth Education in Tanzania cha jijini Mwanza kinachomilikiwa na kanisa la FPCT  alieleza dhamira yake ni kuleta mageuzi ya kimaendeleo katika wilaya hiyo.
"Ndugu zangu Sikonge inazo fursa nyingi za kimaendeleo, kinachotakiwa ni usimamizi mzuri wa fursa hizo kwa kutatua changamoto zilizopo katika sekta mbalimbali ikiwemo ufugaji, maji, elimu na afya’, alisema.
Alisema fursa nyingine ya kimaendeleo iliyoko wilayani humo ni ufugaji nyuki, hivyo akabainisha kuwa ataongeza hamasa kubwa zaidi kwa wananchi na wadau wengine kujitokeza kuwekeza katika hilo ili sekta hiyo pia ilete mageuzi ya kiuchumi kwa wananchi wa Sikonge.
Akizungumza katika mkutano huo Mwenyekiti wa CHADEMA wilayani humo Lucas Kiberenge alisema chama hicho kwa kushirikiana na vyama vyote vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) wamejipanga kulitwaa jimbo hilo kwani CCM wameshindwa kusimamia maendeleo ya wananchi ipasavyo.
Walisema ushindi mkubwa wa wenyeviti wa mitaa na vitongoji waliopatakatika uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika mwezi Desemba mwaka jana ni dalili nzuri za kukubalika wilayani humo na hiyo ni salaamu tosha kwa mbunge huyo na CCM yake, na sasa wanajipanga vizuri zaidi ya hapo.

No comments:

Post a Comment