Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Saturday, 6 June 2015

KIKUNDI CHA MUZIKI CHAPATIWA SH 200,000

Na Hastin Liumba, Tabora
KAMANDA wa umoja wa vijana wa CCM (UVCCM) Kata ya Gongoni, Kessy Sharrif Abdarahaman amekabidhi sh 200,000 kikundi cha muziki wa dansi cha Tabora Music Association (TMA) kwa ajili ya kujiendeleza na ujasiliamali na kilimo.

Kikundi hicho kilianzishwa mwaka 2015 kiajishughulisha na kazi za muziki katika sherehe mbalimbali,kilimo cha umwagiliaji na ujasiriamali.
Sharrrif alikabidhi fedha hizo katika hafla fupi ya uzinduzi wa shina la CCM katika kata ya Gongoni shina ambalo lina vijana 84 wanaume wakiwa 53 na wasichana 31.
Aidha Sharrf alisema ametoa fedha hizo kwa ajili ya vijana hao kujiendeleza kimuziki na kufanya kazi mabalimbali ambazo zitawaingizia kipato.
Hata hivyo aliwataka vijana hao kuacha kutumika katika makundi ya kisiasa yenye maslahi binafsi kwani yana athari kubwa kwa jamii.
Alisema muziki ni ajira na kwamba wanapaswa kujipanga vyema ili walitumikie vyema taifa kupitia muziki, ujasiriamali na kilimo.
Katika hatua nyingine Sharrif aliwataka vijana hao kuhakikisha wanajiandakisha kwenye daftari la wapiga kura ili wapate nafasi na haki yao kimsingi ya kupiga kura.
“Jiandikisheni kwenye daftari hilo ili mpate silaha ya kuchagua viongozi makini hapo 2015 kwani kujiandikisha ndiyo silaha ya kuchagua viongozi makini,” alisema Sharrif.
Awali akisoma risala yao Juma Hamis kundi hilo la muziki lina changamoto kadhaa ambazo ni kushindi kurekodi kazi zao kutokana na gharama kubwa.
Alitaja nyingine ni kuomba elimu toka baraza la sanaa Taznania (BASATA) na kuanzishwa kwa ofisi kila wilaya lakini gharama ni kubwa.
Aidha Hamis alitaja nyingine ni gharama za kazi kilimo cha umwagiliaji kuwa kubwa hivyo wanaomba kupewa sapoti toka kwa viongozi.

No comments:

Post a Comment