Maulid Dilunga
Na Daniel Mbega
Zamani
kulikuwa hakuna ustaa wala nini katika suala la maamuzi, tofauti na sasa ambapo
wachezaji wakisifiwa kidogo wanavimba vichwa na kujiona bila wao timu haziwezi
kufanya vizuri.
Ikitokea
mamlaka husika zikachukua hatua, basi utawaona mashabiki wakishika bango na
kuwatetea wachezaji hao bila kutambua kwamba nidhamu ndio msingi wa mafanikio
katika michezo. Mashabiki wanaweza kuwatukana makocha na viongozi na siyo ajabu
wakiwasingizia kwamba ‘huenda wamenyang’anyana mademu’ mitaani ndiyo maana
kocha ama kiongozi anamchukia mchezaji husika.
Utoro
katika kambi za timu zetu limekuwa jambo la kawaida siku hizi, ulevi na uvutaji
wa bangi ni mambo yaliyotawala, lakini zamani haikuwa hivyo. Zamani hawakujali
umaarufu wako wala nini, sheria ilikuwa msumeno.
Mnamo
Desemba 21, 1971 Mkutano wa Chama cha Soka Tanzania (FAT) na kile cha Zanzibar
(ZFA) uliofanyika Unguja uliamua kumfungia kucheza soka miaka miwili mshambuliaji
wa Yanga na Taifa Stars Maulid Bakari Dilunga kutokana na utovu wa nidhamu.
Ilielezwa
kwamba, Dilunga alitoroka kwenye kambi ya timu hiyo iliyokuwa Jeshi la Wokovu
na kwenda kulewa na kucheza disko kwa siku mbili, na hivyo siku timu ya taifa
ilipoondoka kwenda Guinea kwa mechi za kirafiki hapo Novemba yeye hakuwepo.
Ikiwa huko
Guinea, Tanzania ilipoteza mechi zake zote mbili ambapo mechi ya kwanza
ilichezwa Novemba 2, 1971 mjini Conakry na wenyeji wakashinda kwa mabao 4-2.
Ziliporudiana
tena mjini humo Novemba 14, 971 Guinea ikapunguza dozi na kuifunga Tanzania
mabao 3-2.
Baadaye adhabu
hiyo ikapunguzwa na Dilunga akarejea uwanjani, hasa baada ya yeye mwenyewe
kuomba radhi.
0656-331974

No comments:
Post a Comment