Msanii na mwanamitindo Jokate Mwegelo (kushoto) akiongea na wadau wa Jukwaa la Sanaa la Baraza la Sanaa la Taifa-BASATA (hawako pichani) mapema wiki hii kwenye ukumbi wa Baraza hilo ulioko Ilala Sharif Shamba jijini Dar es Salaam. Wengine kutoka kulia ni mbunifu wa mavazi maarufu nchini Asia Idarous na Katibu wa Chama cha Waandishi wa habari za Sanaa na Utamaduni (CAJAtz), Hassan Bumbuli.
2Mbunifu wa mavazi maarufu nchini Asia Idarous (Kulia) akisisitiza jambo mapema wiki hii wakati akiwasilisha mada kwenye Jukwaa la Sanaa la Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) katika Ukumbi wa Baraza hilo ulioko Ilala Sharf Shamba jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha kutoka kushoto ni Mwanamitindo Jokate Mwegelo na Katibu wa CAJAtz Hassan Bumbuli.
3Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Godfrey Lebejo akipiga marimba ya kigogo mapema wiki hii kwenye Jukwaa la Sanaa la BASATA linalofanyika kila Jumatatu mara mbili kwa mwezi kwenye ukumbi wa Baraza hilo ulioko Ilala Sharif Shamba jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia kushoto kwake ni Mwanamitindo Jokate Mwegelo, Katibu wa CAJAtz Hassan Bumbuli na mbunifu mavazi Asia Idaorus.
4Katibu wa Chama cha Waandishi wa habari za Sanaa na Utamaduni (CAJAtz) Hassan Bumbuli (Katikati) akisisitiza jambo mbele ya wadau wa Sanaa (hawako pichani) kwenye Jukwaa la Sanaa la BASATA linalofanyika mara mbili kwa mwezi siku ya Jumatatu kwenye Ukumbi wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ulioko Ilala Sharif Shamba. Kulia ni Mbunifu mavazi Asia Idarous na mwanamitindo Jokate Mwegelo.
5Msanii mkongwe wa Sanaa za majukwaani nchini Kasim Mbelemba maarufu kama Mzee Jangala (Mwenye bhalagashia) akifuatilia kwa makini mjadala kwenye Jukwaa la Sanaa la BASATA mapema wiki hii.
Mdau wa Sanaa akichangia mada kwenye Jukwaa la Sanaa mapema wiki hii huku baadhi ya wadau wakisikiliza ka makini.
Sehemu ya wadau wa Sanaa waliohudhuria programu ya Jukwaa la Sanaa mapema wiki wiki kwenye Ukumbi wa BASATA ulioko Ilala Sharif Shamba jijini Dar es Salaam.
Na
Mwandishi Wetu
Baraza la Sanaa la Taifa
(BASATA) limetoa wito kwa wasanii kuacha tabia ya kulewa umaarufu na kuchukia
pale wanapokosolewa kwani kazi yoyote ya Sanaa lazima ikosolewe ili iwe bora na
yenye kuvutia.
Wito huo umetolewa mapema
wiki hii na Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Godfrey Lebejo Mngereza wakati
akizungumza kwenye Jukwaa la Sanaa la BASATA linalofanyika kwa mwezi mara mbili
siku ya Jumatatu kwenye Ukumbi wa Baraza hilo ulioko Ilala Sharif Shamba jijini
Dar es Salaam.
Alisema kuwa wasanii
wafurahie wanapokosolewa kwani msanii yeyote duniani lazima atenge muda wa
kuiwasilisha kazi yake kwa hadhira kwa ajili ya kusikilizwa au kuangaliwa na
hatimaye kukosolewa na kutolewa mawazo ya wadau kabla haijaenda sokoni rasmi.
“Kukosolewa kwa msanii ni
sehemu ya kazi. Wasanii wengine hulipa fedha nyingi kwa ajili ya kukosolewa na
kuboreshewa kazi zao. Hapa kwetu wasanii wanakosolewa bure, wanakasirika,
wanamwona adui anayewakosoa” aliongeza Lebejo.
Awali wakiwasilisha mada iliyohusu
Umuhimu wa msanii kutumia umaarufu
kukuza pato kwa nyakati tofauti kwenye Jukwaa hilo, mbunifu wa mavazi
maarufu nchini Asia Idarous na mwanamitindo Jokate Mwegelo kwa pamoja
walisisitiza umuhimu wa wasanii kuwa na malengo, bidii, uaminifu na kutengeneza
kazi zenye ubora.
Jokate alisema kwamba amefika
hapo alipo kutokana na kuzingatia uhusiano mwema katika kazi, kujitangaza,
kujituma, kujiwekea akiba na kujenga mtandao mzuri wa kikazi na wadau
mbalimbali ndani na nje ya nchi pia kujenga umaarufu mzuri usiyo na maadili
mabovu.
“Kupata umaarufu si kwa
mteremko. Si kila umaarufu ni mzuri. Wasanii lazima wabuni kazi nzuri na zenye
maadili ili zionekane na kupendwa. Tusibuni vitu vibaya au sisi wenyewe
kujinadi kwa vitu vibaya” alisisitiza Jokate.
Alizidi kueleza kwamba
hakuna kitu cha muhimu kwa msanii kama uvumilivu , kuepuka makundi yasiyo na
tija na zaidi kuwa karibu na watu wenye mafanikio katika kazi zao ili kuiga
yale yaliyo bora kwa ajili ya kukuza uchumi na pato.
No comments:
Post a Comment